Sunday, September 2, 2012

Robin Van Persie apiga hat-trick na kuiokoa Man Utd na kichapo

Hat-trick ya kwanza kwa Robin Van Persie kama mchezaji wa Manchester United ilikuwa chachu ya ushindi kwa timu hiyo ya upande mwekundu wa Manchester ambapo alifunga magoli mawili katika dakika za majeruhi.Matokeo hayo yenye maumivu makubwa kwa Southampton waliokuwa wakitazamia kuangusha kigogo mmojawapo wa ligi ya Uingereza yaliwasaidia Manchester United kupanda hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi ya Uingereza wakati ligi hiyo ikienda kwenye mapimziko mafupi ya wiki 2 ya mechi za kimataifa.Man Utd ilishinda kwa magoli 3-2.

No comments:

Post a Comment