Tuesday, September 18, 2012

Matokeo UEFA Champions League(Matchday 1)

Jumanne 18/09/2012


Magoli toka kwa Lucho Gonzalez na Steven Defour yameihakikishia Porto ushindi wa goli 2 - 0 dhidi ya Dinamo Zagreb.Dinamo wameendelea kupoteza mechi za makundi katika mashindano haya baada ya kutopata hata pointi moja toka kwenye kundi lao msimu uliopita.


PSG wameanza vizuri mashindano haya hatua ya makundi baada ya kuwaliza Dynamo Kyiv magoli 4 - 1.Magoli ya PSG waliokua nyumbani yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic (pen),Thiago Silva,Alex na la mwisho Javier Pastore.Bao la kufutia machozi la Dynamo lilifungwa na Miguel Veloso.


Arsenal wameanza vizuri msimu huu na kufikia mechi tano bila kufungwa huku wakipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Montpellier ugenini.Magoli ya Arsenal yalifungwa na Lucas Podolski pamoja na Gervinho wakati lile la Montpeller lilifungwa na Younes Belhada.


Malaga walikua washindi dhidi ya Zenit St.Petersburg kwa magoli 3 - 0 toka kwa Isco magoli mawili na pia mkogwe Javier Saviola alijipatia bao moja.


Baada ya kuanza vibaya ligi ya Italia (Serie A) jana AC Milan walianza na suluhu ya bila kufungana dhidi ya Anderletch.Milan walikua nyumbani.


Borrusia Dortmund ambao ni mabingwa wa zamani wa kombe hili walianzia vizuri uwanja wa nyumbani kwa ushindi wa goli lililofungwa na Robert Lewandowski dhidi ya Ajax.Katika mechi ya kundi D.Naamini ni kundi gumu zaidi msimu huu.


Real Madrid ambao ni mabingwa wa kihistoria wa kombe la mabingwa la UEFA jana walithibitisha ubabe wao walipowaliza Manchester City magoli 3-2 huku magoli matatu ya mechi hiyo yakifungwa dakika za majeruhi na kuupa mchezo huo msisimko wa kipekee.Magoli ya Real yalifungwa na Ozil,Benzema na Ronaldo na yale ya Manchester City yalifungwa na Dzeko na Kolarov.


Schalke walimaliza hadithi ya timu za kundi B kushinda ugenini na wao walipojipatia ushindi wa goli 1 - 2 wakiwafunga Olympiacos nyumbani kwao.Hii imewafanya walingane kwa kila namna na Arsenal na kuongoza kundi B pamoja.Magoli yalifungwa na Benedict Howedes na Klaas Jan Huntelaar.Goli la Olympiacos lilifungwa na Djamel Abdoun.








No comments:

Post a Comment