Monday, November 12, 2012

Djokovic amshinda Federer kwenye fainali za ATP World Tour

Habari kubwa katika ulimwengu wa michezo toka jana ni ushindi wa Novak Djokovic dhidi ya Roger Federer katika fainali iliyokuwa imejaa upinzani wa hali ya juu.
Kwa wale wajuzi wa Tennis haya ni mashindano ya ndani (Indoor) na unapoona mtu kashinda kwa pointi 7-6,7-5 unjua kwamba mechi ilikuwa ngumu.

 Djokovic akiwa amebeba kombe lake la fainali za ubingwa wa dunia za ATP.



Hapa ni baada ya kushinda point ya mwisho iliyomaliza mpambano mkali kati ya wababe hao


Sunday, November 11, 2012

Matokeo ya Ligi kuu ya Hispania(La Liga)-Matchday 11

Real Betis               1 -2           Granada
Rayo Vallecano      3 - 2           R.C. Celta
Espanyol                0 -3            Osasuna
Zaragoza                5 -3            Deportivo
Malaga                   1 - 2           Real Sociedad
Valladolid                1 - 1          Valencia
AC Bilbao               2 - 1          Sevilla
Mallorca                  2 - 4          Barcelona
Atletico Madrid       2 - 0           Getafe
Levante                   1 - 2           Real Madrid

Mou:My team is commited,ambitous and with a desire to win and to improve.


Matokeo Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

Ijumaa 09/11/12
Mainz                   2 - 1       Nurnberg

Jumamosi 10/11/12
Bayern                  2 - 0      Frankfurt
Schalke 04            2 - 1      Bremen
Freiburg                0 - 0      Hamburg
Augsburg              1 - 3      Dortmund
Dusseldorf            1 - 1      Hoffenheim

Jumapili 11/11/12
Wolfsburg              3 -1       Leverkusen
Stuttgart                2 - 4       Hannover
Greuther Furth       2 -4       M'gladbach


Kiungo mchezeshaji wa Wolfsburg akishangilia goli.Alikuwa siri ya mafanikio yao jana walipoifunga Leverkusen.

Matokeo Ligi kuu ya Italia(Serie A)

Atalanta wakiwa nyumbani walimaliza mfululizo wa ushindi kwa Inter Milan baada ya kuifunga magoli 3 - 2.

Katika viwanja vingine:
Cagliari       0 - 0       Catania
Chievo        2 - 2       Udinese
Genoa         2 - 4       Napoli
Lazio           3 - 2       Roma
Milan           1 - 3       Fiorentina
Palermo       2 - 0       Sampdoria
Parma          0 - 0       Siena
Pescara        1 - 6       Juventus
Torino          1 - 0       Bologna

Juventus wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne.Inter Milan wiki iliyopita waliiharibia Juventus rekodi ambapo walikuwa wanatafuta rekodi ya kucheza mechi 50 za mashindano bila kupoteza mchezo.Ligi hii inazidi kuwa tamu!

Matokeo ya Ligi kuu ya Uingereza 11/11/2012

Pichani ni Luis Suarez aliyesawazisha bao dakika ya 73 dhidi ya Chelsea na kuzifanya Chelsea na Liverpool kutoshana nguvu kwa kufungana goli 1 - 1 matokeo yaliyoishusha Chelsea mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi hiyo.bao la Chelsea lilifungwa na John Terry dk20.

Man City                   2 - 1           Tottenham
Sergio Aguero 65                         Steven Caulker 21
Edin Dzeko 88

Newcastle                 0 - 1         West Ham Utd
                                                   Kevin Nolan 37

Saturday, November 10, 2012

Matokeo ya Ligi kuu Uingereza(EPL)-Matchday 11

Arsenal                        3 - 3         Fulham
Giroud 11 , 69                              Berbatov 29,67 pen
Podolski 23                                  Kacaniklic 40







Everton                        2 - 1         Sunderland
Fellaini 76                                     Johnson 45+1
Jelavic 79

Reading                        0 - 0         Norwich

Southampton                1 - 1          Swansea
Schneiderlin 64                              Nathan Dyer 73

Stoke                           1 - 0          QPR
Charlie Adam 52

Wigan                           1 - 2         West Brom
Arouna Kone 44                           James Morrison 31
                                                     Gary Caldwell 43(og)

Aston Villa                    2 -3          Man Utd
Andreas Weimann 45+1                Chicharito 58,87
50                                                 Ron Vlaar 63(og)


Friday, November 9, 2012

Ratiba Ligi Kuu ya Hispania

Baada ya mchezo wa jana usiku kati ya Real Betis na Granada (Matokeo 1 - 2) mechi zingine weekend hii Hispania kwenye La Liga zinahusisha:

Jumamosi 10/11/2012
Saa 1 usiku        Rayo Vallecano  vs       R.C. Celta
Saa 3 usiku        Espanyol            vs       Osasuna
Saa 5 usiku        Zaragoza            vs       Deportivo
Saa 7 usiku        Malaga               vs       Real Sociedad

Jumapili 11/11/2012
Saa 9 mchana    Valladolid            vs       Valencia
Saa 1 usiku        A.C. Bilbao        vs       Sevilla
Saa 2:50 usiku    Mallorca            vs       Barcelona
Saa 4:45 usiku    Atletco Madrid  vs       Getafe
Saa 6:30 usiku    Levante              vs      Real Madrid

Ratiba Ligi Kuu ya Uingereza weekend hii

Jumamosi 10/11/2012
11 jioni            Arsenal           vs       Fulham
      -                Everton          vs      Sunderland
      -                Reading          vs      Norwich
      -                Southampton  vs       Swansea
      -                Stoke             vs       QPR
      -                Wigan            vs      West Brom
1:30 usiku        Aston Villa     vs       Man Utd

Jumapili 11/ 11/2012
9:30 mchana    Man City        vs       Tottenham
11:00 jioni        Newcastle      vs      West Ham Utd
12:00Jioni        Chelsea          vs       Liverpool

Sunday, November 4, 2012

Matokeo Ligi ya Hispania (La Liga)-Matchday 10

Diego Pablo Simeone kocha waliokuwa vinara wa ligi ya Uhispania kwa kulingana pointi na Barcelona.Weekend hii wamepigwa na Valencia inayotafuta pointi kwa nguvu zote.

Malaga                1 - 2        Rayo Vallecano
FC Barcelona      3 - 1        R.C Celta
Real Madrid        4 - 0        Zaragoza
Valencia              2 - 0        Atletico Madrid
Real Sociedad    0 - 1         Espanyol
Deportivo           1 - 0         Mallorca
Osasuna             0 - 1         Valladolid
Granada             1 - 2         Athletic Club
Sevilla                0 - 0          Levante

Imebaki mechi moja tu takayochezwa usiku wa leo kati ya
Getafe                 vs            Real Betis

Matokeo Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga)-Matchday 10

Ijumaa 02/11/2012
E.Frankfurt     1 - 1    Greuther Furth

Jumamosi 03/11/2012
Dortmund       0 - 0      Stuttgart
M'gladbach    1 - 1      Freiburg
Hannover       2 - 0      Augsburg
Nurnberg       1 - 0      Wolfsburg
Hoffenheim    3 - 2       Schalke 04
Hamburg       0 - 3       FC Bayern

Jumapili 03/11/2012
Leverkusen    3 - 2      Dusseldorf
Bremen          2 - 1      Mainz

Matokeo Ligi kuu Uingereza-Matchday 10

Jumamosi 03/11/2012
West Ham       0 - 0           Man City
Fulham            2 - 2           Everton
Norwich          1 - 0           Stoke
Sunderland       0 - 1          Aston Villa
Swansea          1 - 1          Chelsea
Tottenham        0 - 1           Wigan
Man Utd          2 - 1           Arsenal

Jumapili 04/11/2012
Liverpool        1 - 1           Newcastle
QPR               1 - 1           Reading

Sunday, October 28, 2012

Matakeo Ligi kuu ya Uingereza(EPL)-Matchday 9

Jumamosi 27/10/2012
Man City            1 - 0      Swansea
Arsenal               1 - 0      QPR
Reading              3 - 3      Fulham
Stoke                 0 - 0      Sunderland
Wigan                 2 - 1      West Ham
Aston Villa          1 - 1      Norwich


Jumapili 28/10/2012
Chelsea               2 - 3     Man Utd
Newcastle           2 - 1     West Brom
Southampton       1 - 2     Tottenham
Everton               2 - 2      Liverpool

Sunday, October 21, 2012

Matokeo EPL weekend hii

Juu ni Manchester City wakishabikia ushindi wao wa Dakika za mwisho za mchezo kwa umahiri wa Edin Dzeko anayeshangilia bila shati Pichani.Alifunga magoli yao yote mawili akitokea benchi.                                                            West Brom  1 - 2  Man City               (Jumamosi 21/10/2012)

Chelsea wameendeleza kazi ya kuuelekea ubingwa kwa kuwacharaza majirani na mahasimu wakubwa wa Arsenal pale London Kaskazini na matokeo yalikuwa
                                                              Tottenham  2 - 4  Chelsea            (Jumamosi 21/10/2012)

Arsenal waliaibishwa na kuondoka Carrow Road na kumbukumbu mbaya ya kufungwa goli moja huku Arsene Wenger akikasirishwa na kulalamikia kiwango kibovu cha timu yake.
                                                           Norwich    1 - 0    Arsenal              (Jumamosi 21/10/2012)
                 
Mechi zingine zilizochezwa siku hiyo matokeo yalikua hivi:
                                                           Fulham          1 - 0    Aston Villa
                                                           Liverpool       1 - 0    Reading
                                                           Man Utd        4 - 2    Stoke City
                                                           Swansea         2 - 1    Wigan
                                                           West Ham      4 -  1    Southampton
                                                           
Jumapili 22/10/2012
                                                            QPR            1 - 1       Everton
                                                            Sunderland   1 - 1       Newcastle
          

Thursday, October 18, 2012

Mechi za weekend hii Ligi Kuu Hispania_La Liga

Espanyol          vs        Rayo
Malaga            vs        Valladolid
Sociedad         vs        A.Madrid
Osasuna          vs        Betis
Valencia          vs        Athletic
Getafe             vs        Levante
Granada          vs        Zaragoza
Sevilla             vs        Mallorca
R.Madrid        vs        Celta
Deportivo       vs        Barcelona

Ratiba ligi kuu Uingereza EPL-Matchday 8

Jumamosi 20/10/2012

Saa(EAT)                             Mechi
10:45 jioni               Tottenham     vs      Chelsea
01:00 usiku             Fulham          vs      Aston Villa
01:00                      Liverpool      vs      Reading
01:00                      Man Utd       vs      Stoke City
01:00                      Swansea       vs      Wigan
01:00                      West Brom   vs       Man City
01:00                      West Ham    vs       Southampton
03:30                      Norwich       vs       Arsenal

Jumapili 21/10/2012

09:30jioni               Sunderland  vs        Newcastle
12:00jioni               QPR           vs        Everton

Sunday, October 7, 2012

Matokeo ligi kuu ya Ujerumani(Bundesliga)-Matchday 7

Ijumaa 05/10/2012
Augsburg                    3 - 1       Bremen

Jumamosi 06/10/2012
Bayern                        2 - 0       Hoffenheim
Schalke                       3 - 0       Wolfsburg
Freiburg                      3 - 0       Nurnburg
Mainz                         1 - 0       Dusseldorf
Greuther Furth            0 - 1       Hamburg

Jumapili 07/10/2012
Munchengladbach      2 - 0       Frankfurt
Stuttgart                     2 - 2       Leverkusen
Hannover                   1 - 1       Dortmund

Matokeo Ligi kuu ya Hispania(La Liga)-Matchday 7

Pichani ni heka heka za hapo jana ndani ya Nou Camp wakati Real walipokua wageni wa Barca na wakatoshana nguvu

Celta                       2 - 0          Sevilla
Rayo Vallecano        2 - 1          Deportivo
Zaragoza                 0 - 1           Getafe
Valladolid                1 - 1           Espanyol
Real Betis                2 - 0          Real Sociedad
Levante                   1 - 0          Valencia
Mallorca                 1 - 2           Granada
Athletic Club           1 - 0           Osasuna
Barcelona                2 - 2          Real Madrid
Atletico Madrid       2 - 1           Malaga

Vettel wins at Suzuka Japanese Grand Prix

Sebastian Vettel amejipa zaidi matumaini ya kuwa bingwa wa dunia kwa mara ya tatu mfululizo katika mashindano ya magari ya langalanga (Formula 1 racing) baada ya kushinda mashindano ya magari hayo ya Japan ambapo alianza akiwa mbele na kushikilia nafasi hiyo hadi mwisho wa mashindano.Inaonekana mamekanika wa Red Bull wamekuwa kazini toka msimu uanze kutengeneza gari bora zaidi kwa ajili ya kumalizia msimu na hayo yalidhihirika katika shukrani zake kwa timu yake baada ya ushindi huo.Katika podium pia alijumuika na dereva wa Ferarri tokea Brazil Felipe Massa pamoja na mjapani Kamui Kobayashi mjapani anayeendeshea timu ya Sauber.Jenson Button alimaliza wa nne na pia Lewis Hamilton wa tano.Anayeongoza mashindano ya Dunia Fernando Alonso alipata ajali na hakumaliza mashindano baada ya kugongwa na Kimi Raikkonen.
Mark Webber dereva mwingine wa Red Bull ambae alianza mashindano akiwa mbele alimaliza wa kumi na moja baada ya kugongwa katika mzunguko wa kwanza tu na mfaransa ambaye amekuja kuwa mashuhuri kwa kugonga wenzake Roman Grosjean.
Gap kati ya Vettel na Alonso kwa sasa ni pointi 4 kukiwa kumebaki mashindano matano tu mwaka huu.


Matokeo ya EPL Matchday 7(07/10/2012)

Pichani beki wa Man Utd Evans akiifungia timu yake goli la kwanza katika uwanja wa Sport Direct Arena ambapo Man Utd wametoka na ushindi wa goli 3 bila majibu.

Southampton       2 - 2      Fulham
Liverpool            0 - 0      Stoke City
Tottenham           2 - 0      Aston Villa
Newcastle           0 - 3      Man Utd

Saturday, October 6, 2012

Matokeo ligi kuu Uingereza EPL 06/10/2012

Pichani Aaron Ramsey katika mojawapo ya heka heka za mechi ya jana ambapo Arsenal walishinda London Derby kwa magoli 1 - 3 wakiwa ugenini Upton park.

Man City        3 - 0        Sunderland
Chelsea          4 - 1        Norwich
Swansea         2 - 2        Reading
West Brom     3 - 2        QPR
Wigan             2 - 2        Everton
West Ham      1 - 3         Arsenal

Theo Walcott kusign mkataba mpya na Arsenal

Theo Walcott ameongelea kuongeza mkataba na Klabu ya Arsenal akisubiria kwa hamu mazungumzo ya mwisho na kusign mkataba mpya wa miaka mitatu ndani ya wiki mbili zijazo na ameelezea kutamani sana kurudi kwenye mipango ya kudumu ya klabu hiyo.Haya yamekuja huku Arsene Wenger akielezea uamuzi wa kumchezesha kuanzia sasa winga huyo mwenye kasi ya ajabu kama mshambuliaji wa kati nafasi anayoipenda sana na inayochezwa na nyota aliyemfanya mchezaji huyo kutua Highbury akitokea Southampton ambaye anasumbua katika ligi ya Marekani Thierry Henry.

Wednesday, October 3, 2012

Matokeo Ligi ya Mabingwa Ulaya(UEFA Champions League)-Matchday 2(03/10/2012)

Gervinho akifanya vitu vyake hapo jana dhidi ya Olympiacos katika uwanja wa Emirates ambapo Arsenal lishinda 3-1.

Group A
Porto                      1 - 0           PSG
(James Rodriguez 83')

Dynamo Kyiv         2 - 0           Dinamo Zagreb
Gusev 3'
Pivaric 33'(o.g)

Group B
Arsenal                  3 - 1           Olympiacos
Gervinho 42'                             Mitroglou 45+1
Podolski 56'
Ramsey 90+4

Schalke                  2 - 2           Montpellier
Draxler 26                                Ait-Fana 13
Huntelaar 53 P                         Camara 90

Group C
Zenit                      2 - 3           AC Milan
Hulk 45+2                                Emanuelson 13
Shirokov 49                              El Shaarawy 16
                                                 Hubocan 75 (og)

Anderlecht             0 - 3           Malaga
                                                Eliseu 45+1,64
                                                Joaquin 57

Group D
Man City               1 - 1           Dortmund
Balotelli 90 P                            Reus 61
    
Ajax                      1 - 4           Real Madrid
Moisander 56                           Cristiano Ronaldo 42,79,81
                                                Benzema 48

Timu zilizotumia pesa nyingi hazikufanya vizuri,wakongwa wameendelea kusumbua Milan ikirudi kwenye ramani baada ya kuanza vibaya Serie A na pia Cristiano Ronaldo anakua mchezaji wa kwanza kufunga Hat Trick kwenye mashindano ya ulaya dhidi ya Ajax kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Amstedam Arena.


Tuesday, October 2, 2012

Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UEFA Champions League)-Matchday 2

RVP akifunga goli la pili kwa Man Utd ugenini jana.

Group E
Juventus                 1 - 1         Shakhtar Donestk
(Bonnuci 25')                          (Alex Teixeira 23')

Nordsjaelland         0 - 4        Chelsea
                                              (Juan Mata 33' 82',David Luiz 79',Ramires 89')

Group F
Valencia                  2 - 0        LOSC Lille
(Jonas 38' 75')

BATE                     3 - 1        Bayern Munich
(Pavlov 23',Rodionov 78',Renan 90+')        (Riberry 90+')

Group G
Spartak Moscow    2 - 3       Celtics
(Emenike 41' 48' Kombarov 71' pen)          (Hopper 12',Samaras 90')

Benfica                   0 - 2       Barcelona
                                             (Alexis Sanchez 6', Fabregas 55')

Group H
CFR Cluj               1 - 2        Man Utd
(Kapetanos 14')                     (RVP 29' 49')

Galatasaray            0 - 2        Braga
                                             (Ruben Mikael 27', Alan 90+')



Sunday, September 30, 2012

Matokeo weekend hii Ligi kuu Ufaransa

Bordeaux wameihariba rekodi ya kutofungwa ya Lyon weekend hii

Matokeo wiki ya 7 ya ligi
Ijumaa 28/09/2012
Stade Rennais      2 - 0        LOSC Lille

Jumamosi 29/09/2012
PSG                    2 - 0         Sochaux
Ajaccio               1- 0           Stade Brestois 29
Evian                   1 - 1         Lorient
AS Nancy           0 - 2         Montpellier
OGC Nice          2 - 2          Bastia
Troyes                0 - 2          Toulouse

Jumapili 20/09/2012
Valenciennes       4 - 1          Marseille
Saint Etienne       0 - 0          Stade Reims
O. Lyonnais        0 - 2          Bordeux

Matokeo Ligi kuu Italia weekend hii(Serie A)

Pichani Diego Milito akishangilia goli lililoipa ushindi Inter dhidi ya Fiorentina waliomaliza mechi wakiwa kumi uwanjani

Matokeo wiki ya 6 ya ligi
Atalanta           1 - 5       Torino
Bologna           4 - 0       Catania
Cagliari            1 - 2       Pescara
Inter                 2 - 1      Fiorentina
Juventus           4 - 1      Roma
Lazio               2 - 1       Siena
Palermo           4 - 1       Chievo
Parma              1 - 1       Milan
Sampdoria       0 - 1       Napoli
Udinese           0 - 0       Genoa

Matokeo Ligi ya Hispania weekend hii

Pichani ni Zubicarai golikipa wa akiba wa Real Sociedad ambaye amechukua nafasi ya golikipa namba moja wa timu hiyo aliyeumia wakati wa mechi ya watani wa jadi tokea jimbo la Catalunya (The Basque Derby) kati ya timu yake na Athletic Club Bilbao


Matchday 6
Valencia            2 - 0       Zaragoza
Malaga             4 - 0       Real Betis
Real Sociedad  2 - 0       Athletic Club
Sevilla              2 - 3       Barcelona
Granada           2 - 1       Celta
Valladolid         6 - 1        Rayo Vallecano
Osasuna           4 - 0        Levante
Real Madrid     5 - 1        Deportivo
Espanyol          0 - 1        Atletico Madrid

Matokeo ya mechi Ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

Pichani Marco Reus wa Borrusia Dortmund akiwatoka mabeki wa timu yake ya zamani ya Borrusia Munchegladbach ambapo alikua chachu ya ushindi wa goli 5 - 0.

Ijumaa 28/09/2012
Dusseldorf          2 - 2 Schalke 04

Jumamosi 29/09/2012
Leverkusen        2 - 0       Greuther Furth
Bremen              0 - 2       FC Bayern
Nurenberg         0 - 2        Stuttgart
Hoffenheim        0 - 0        Augsburg
Hamburg           1 - 0        Hannover
Dortmund          5 - 0        M'gladbach

Jumapili 30/09/2012
Frankfurt           2 - 1        Freiburg
Wolfsburg         0 - 2         Mainz

Saturday, September 29, 2012

Matokeo Ligi kuu ya soka Uingereza-Matchday 6






Saturday 29/09/2012
Arsenal            1 - 2      Chelsea
Everton           3 - 1       Southampton
Fulham            1 - 2       Man City
Norwich          2 - 5       Liverpool
Reading           2 - 2       Newcastle
Stoke              2 - 0       Swansea
Sunderland      1 - 0       Wigan
Man Utd         2 - 3       Tottenham

Sunday 30/09/2012
Aston Villa      1 - 1      West Brom

Yanga yapata kocha mpya

Ernstus Wilhelmus Johannes Brandts amesaini mkataba wa kuifundisha timu ya soka ya Klabu ya michezo ya Yanga (Dar-es-salaam Young Africans) ama anavyoonekana pichani.Makamu mwenyekiti Clement Sanga akielekeza jambo kuhakikisha mambo yanafanyika kwa mujibu wa taratibu.Ni Kocha wa pili kwa Yanga msimu huu na sijui kama atakaa.

Chelsea yashinda Battle of London

Kwa mara ya kwanza Arsenal wamepoteza mchezo msimu huu walipokutana na Chelsea mapema leo kwenye uwanja wa Emirates matokeo haya yakiwa ni magoli yaliyotokana na mipira ya adhabu.Arsenal walionyesha udhaifu katika kulinda dhidi ya mipira ya adhabu na pengine lilikuwa kosa kumchezesha Laurent Koscielny leo badala ya Per Metersacker.
Chelsea ambao wamezidi kujiongezea kasi ya kuuelekea ubingwa wa Ligi msimu huu walitawala zaidi nafasi ya kiungo na pengine pengo la Abou Diaby lilikuwa dhahiri kwa Arsenal.
Magoli yalifungwa na Fernando Torres na Juan Mata kwa Chelsea na lile la Arsenal kufungwa na Gervinho.Matokeo ya mwisho Arsenal 1 - 2 Chelsea.mechi nyingine za ligi ya Uingereza EPL zinaendelea kwa sasa.

Sijui wabongo mnaijua Ryder Cup?


Ryder Cup ni kikombe mashindano ya tennis yanayochezwa kila baada ya miaka miwili kati ya timu ya Marekani dhidi ya timu ya mataifa ya Ulaya na husimamiwa kwa pamoja kati ya chama cha mchezo wa golf kiprofesheno cha Marekani (PGA of America) na kile kinachosimamia mchezo huo kiprofesheno Ulaya PGA European Tour.Washiriki hupatikana kwa viwango vyao na wachache huchaguliwa na Nahodha wa kila timu.
Cha kushangaza mwaka huu kwenye mashindano haya ni uamuzi wa jana wa Nahodha wa timu ya Marekani kutomshirikisha katika hatua za Mwisho Tiger Woods ambaye siku zilizotangulia alishindwa.Na hii ni pamoja na kwamba Marekani inaongoza ikiwa na advantage ya 5-3 ambapo wana nafasi kubwa ya kushinda kikombe cha mwaka huu.Nahodha huyo Davis Love III amesema amefanya hivyo kumpumzisha baada ya siku mbili za mwanzo akielezea kiwanja wanachotumia cha Medinah Country Club,Medinah,Illinois kuwa ni kigumu na hangependa wachezaji wa timu yake kuchoka sana kwa kucheza mechi 5 katika kipindi cha mashindano hayo.Mashindano hayo yataendelea kesho baada ya mapumziko ya leo.

Lewis Hamilton kuelekea Mercedes msimu ujao

Imethibitika kwamba Lewis Hamilton ataihama timu yake ya McLaren msimu ujao na hapo jana timu hiyo imemtangaza raia wa Mexico anayeendeshea magari ya langalanga ya timu ya Sauber kwa sasa Sergio Perez kama mbadala wake msimu ujao.
Martin Whitmarsh ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu(CEO) wa McLaren Racing ametangaza jana akielezea kufurahishwa kwake na ujio wa bwana Perez kwenye timu yake msimu ujao na kusisitiza hakuna dereva aliye mkubwa kuzidi timu.

Wednesday, September 26, 2012

Kombe la Ligi Uingereza raundi ya nne

Raundi ya nne inatazamiwa kuchezwa Okatoba 29 mwaka huu ambapo mechi kubwa kabisa inatazamiwa kuwa kati ya Chelsea na Manchester United.Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:

Sunderland      vs        Middlesbrough
Swindon          vs        Aston Villa
Wigan              vs        Bradford
Leeds              vs        Southampton
Norwich          vs        Tottenham
Liverpool         vs        Swansea
Chelsea           vs        Man Utd
Reading           vs        Arsenal

Arsenal waanza mashindano ya Kikombe cha Ligi kwa kishindo

Hapo jana Arsenal ilianza mashindano ya Kombe La Ligi za chama cha soka cha Uingereza kwa kishindo baada ya kuishindilia timu ya Coventry City magoli 6 - 1 magoli matano ya Arsenal yakifungwa katika kipindi cha pili.Katika hali ya kutia hamasa kwa Arsenal ni mchezaji Olivier Giroud kufunga goli lake la kwanza akiwa mchezaji wa Arsenal wakati pia kulikuwa na magoli kutoka kwa Ox,Asharvin,Theo Walcott aliyefunga mawili pamoja na beki Ignasi Miquel.Goli la kufutia machozi la Coventry City lilifungwa na Callum Ball na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 6 - 1 ambapo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger  aliwachezesha zaidi wachezaji wa timu ya vijana pamoja na wale ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.Baada ya mchezo alisifia umakini wa wachezaji wake na pia kusifia kiwango chao.Arsenal imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo msimu huu ikiwa imeruhusu magoli manne tu kwenye mashindano yote.
Katika raundi ya nne inayoteazamiwa kuchezwa tarehe 29 Oktoba Arsenal itakua wageni wa Reading kushindania kuingia Robo Fainali ya mashindano haya.

Monday, September 24, 2012

Unajua historia ya Capital One Cup?

Huu ni msimu wa 53 wa kombe hili linalojulikana pia kama kombe la ligi (The Football League Cup) na msimu uliopita tulilijua zaidi kwa jina la Carling Cup kutokana na Carling kuwa ndio wadhamini wa chama cha mpira wa miguu Uingereza mwaka huo lakini udhamini mwaka huu umehamia kwa Benki nyingine ya Capital One na kwa sababu hiyo mashindano kubadilishwa jina.Hiki ni kikombe cha pili kwa umaarufu katika michuano ya mtoano huko Uingereza ambapo mshindi huenda kucheza katika ligi ya bara la Ulaya ya Europa na ni nafasi pekee finyu kwa vilabu vichanga nchini humo kuweza kushiriki mashindano ya Ulaya hasa ukichukulia timu kubwa huwa zinachezesha timu zake za vijana na hivyo kuongeza uwezekano wa timu ndogo kushinda hii ikisababishwa na udogo wa zawadi ya mashindano haya ya pauni 100,000 kwa mshindi wa kwanza na 50,000 kwa mshindi wa pili tofauti na Kombe la FA ambalo zawadi ya kwanza huwa ni pauni mil 2.Pia ukweli kwamba timu kubwa zenye nafasi kubwa ya kushiriki UEFA Champions League na Europa League kupitia nafasi zao kwenye ligi huwa hazioni sababu ya kugombea sana kikombe hiki.
Capital One Cup inashirikisha timu 92 bora za Uingereza ambapo timu zote 92 zinashiriki katika mchezo wa mpira wa miguu ngazi ya Ligi nchini Uingereza kuanzia Ligi kuu mpaka daraja la 3 la huko.
Timu kubwa zinazoshiriki mashindano ya Ulaya huanzia hatua ya mzunguko wa tatu wakati timu zote zilizobaki huanzia raundi ya kwanza.
Mashindano haya yalianzishwa msimu wa mwaka 1960-61 na Aston Villa ndo walikuwa washindi wa mara ya kwanza.Kwa sasa bingwa mtetezi ni Liverpool walioshinda kikombe hiki msimu uliopita.Yalianzishwa hasa kama mashindano ya kati ya wiki Uingereza hasa baada ya timu nyingi kuweka taa kwenye viwanja vyake na kuongeza uwezekano wa kuchezwa kwa mechi za jioni katikati ya wiki hasa kipindi ambacho hakukuwa na mechi nyingi za katikati ya wiki za Ulaya kwa timu za Uingereza.Mzunguko wa 3 unatazamiwa kuchezwa leo na kesho ambapo timu nyingi kubwa zinatazamiwa kama kawaida kuchezesha vikosi vyao vya vijana.Mechi ngumu kabisa inatazamiwa kuwa

Manchester United   vs     Newcastle           (26/09/2012)
Manchester City       vs     Aston Villa          (25/09/2012)

Mechi nyingine zinazohusisha timu kubwa Uingereza zitakua:

25/09/2012
West Ham               vs      Wigan
Leeds Utd               vs      Everton
Chelsea                   vs      Wolves

26/09/2012
QPR                       vs      Reading
West Brom              vs      Liverpool
Carlisle                    vs      Tottenham
Arsenal                    vs     Coventry City