Sunday, July 13, 2014

Kurudi Hewani

Mtanisamehe wadau wote maana nilipoteza password ya akaunti yangu hiyo kushindwa kuweka updates na kuwajuza yanayojiri katika ulimwengu wa michezo.Kuanzia sasa nitajitahidi kufanya hivyo...

Mwenyekiti

Saturday, March 30, 2013

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania BaraKabla ya matokeo ya mechi za March 30.
Rank
Teams
Played
Wins
Draw
Lost
GD
Points
1
Young Africans
20
15
3
2
25
48
2
Azam FC
21
13
4
4
20
43
3
Simba SC
20
9
7
4
11
34
4
Kagera Sugar
21
9
7
5
5
34
5
Mtibwa Sugar
21
8
8
5
4
32
6
Coastal Union
21
8
8
5
4
32
7
Ruvu Shooting
20
8
5
7
2
29
8
JKT Oljoro
21
6
7
8
-3
25
9
Mgambo Shooting
21
7
3
11
-6
24
10
JKT Ruvu
20
6
4
10
-13
22
11
Prisons FC
21
4
8
9
-9
20
12
Police Moro
21
3
8
10
-10
17
13
Toto African
21
3
8
10
-12
17
14
African Lyon
21
4
4
13
-18
16

Matokeo Ligi kuu ya Ujerumani-Bundesliga Matchday 27

Leo Bayern Munich wameisogelea zaidi ndoto yao ya kuweka historia huku wakikaribia ubingwa wa ligi ya Ujerumani mashuhuri kama Bundesliga kwa kuwapiga Hamburg kwa goli 9 - 2.Pichani juu Claudio Pizzaro akifunga mojawapo ya magoli hayo 9.

                          Stuttgart      1   -   2     Dortmund
                          Freiburg      2   -   0     Munchegladbach
                      Dusseldorf      1   -   4     Leverkusen
                        Augsburg      0   -   2     Hannover
                             Mainz      1   -   1     Bremen
                     Schalke 04      3   -   0     Hoffenheim
                     FC Bayern      9   -   2     Hamburg

Matokeo ligi kuu Uingereza Matchweek 31

Manchester United wameendeleza wimbi la ushindi na kujikita kwenye usukani wa Ligi Kuu ya Uingereza(EPL) baada ya ushindi wa goli moja lilitokana na kazi nzuri ya Robin van Persie na kumsabisha Titus Bramble wa Sunderland ajifunge kama inavyoonekana pichani juu.

                                         Sunderland    0   -    1 Man Utd
                                                                           Bramble 27 og


Manchester City leo nao hawakubaki nyuma kushikilia vizuri zaidi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kutoa adhabu kali ya magoli 4 kwa Newcastle Utd.Pichani juu Silva akifunga goli la pili.

                                    Man City       4     -      0     Newcastle
                                    Tevez 41
                                    Silva 45+2
                                    Kompany 56
                                    Perch 69 og

Chelsea wamekutana na kisiki cha Southampton leo na wakala kipigo cha goli 2 - 1 ugenini.Pichani juu Rodriguez akimalizia mambo dhidi ya Cech.

                                     Southampton   2   -     1    Chelsea
                                     Rodriguez 23                    John Terry 33
                                     Rickie Lambert 35


Na the Gunnerz leo waliamka toka usingizini na kuwaweka mkiani mwa EPL timu ya Reading kwa kuwafunga magoli manne huku wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huku Kirean Gibbs akicheza mechi yake ya 100 kwa timu hiyo ya kaskazini ya London.Mnamo dakika ya saba ya mchezo uwanja wote ulisimama na kupiga makofi kama heshima ya kumbukumbu ya mchezaji namba saba wa zamani anayekumbukwa zaidi na aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa (Hodgkin's Lymphoma) mwaka 2001 maarufu kama Rocky 7 (David Rocastle)

                                    Arsenal      4         -        1      Reading
                                    Gervinho  11
                                    Carzola 48
                                    Giroud 68
                                    Arteta 77 pen


Matokeo ya michezo mingine ni kama ifuatavyo:

                              Swansea      1    -     2        Tottenham
                              West Ham    3    -    1        West Brom
                              Wigan          1    -     0        Norwich 
                                   Thursday, March 14, 2013

Saturday, March 9, 2013

Marakana yafurika

Pichani juu mojawapo ya viwanja vitakavyotumika katika Kombe la Dunia Brazil mwakani ukiwa umefurika maji baada ya mvua kubwa zinazoendelea Brazil.Uwanja huu unatazamiwa kutumiwa kwenye mechi ya kirafiki Juni 2 kati ya Brazil na Uingereza.Umewahi kusemwa kuwa uwanja mkubwa zaidi duniani na kwa sasa unafanyiwa ukarabati ambapo paa limeezuliwa upande mmoja,viti viliondolewa na sasa umebainika una tatizo la kufurika maji hii ikiwa mara ya pili hili kurokea.Ni changamoto kubwa kwa maandalizi ya kombe la dunia mwakani ambapo ulitazamiwa kutumika kwenye ufunguzi na mechi ya mwisho/fainali ya mashindano

Golikipa afungwa miaka 22 jela kwa kumuua mpenzi wake

Mmojawapo wa waliokuwa magolikipa bora zaidi kwenye ligi kuu ya Brazil na aliyekua nahodha wa  timu ya Flamengo ya huko inayoshiriki Ligi kuu ya Brazil juzi alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake wa zamani na kisha kuukatakata mwili wake na kuwalisha mbwa.
Bruno Fernandes de Souza alikuwa katika nafasi nzuri kuitwa kwenye timu ya taifa ya Brazil na pia kusajiliwa kwa mkataba mkubwa na timu ya AC Milan wakati siri za mauaji haya ya kutisha zilipoanza kuibuka Brazil.Alituhumiwa kumuua mpenzi wake aliyekua pia mwanamitindo nchini humo baada ya kumlaghai na kumualika katika shamba lililo katika jimbo la Minas Gerais ambako binti huyo aliuawa na kisha kukatwakatwa vipande vipande na maiti yake kulishwa mbwa waliokuwa maeneo hayo.Maiti yake haijapatikana hadi leo hii.
Mwanamitindo Eliza Samudio pichani juu aliwahi pia kutekwa siku za nyuma akiwa na ujauzito wa Bruno na kushawishiwa pamoja na kulazimishwa kuitoa mimba hiyo ambapo alikataa na kupeleka mashitaka polisi.Wakati wa kesi hiyo hakuonekana na katika uchunguzi ndo yalipoibuka haya ya mauaji ya kutisha ambapo Bruno aliwashirikisha baadhi ya ndugu zake,marafiki wa karibu,mke wake wa zamani na hata mmojawapo wa wachumba zake.
Bruno amepewa hukumu ndogo kwa sababu ya kushirikiana kwake na polisi na pia kutubu kushiriki mauaji hayo mahakamani ingawa amekua akisisitiza kwamba mrembo huyo aliuawa kwa bahati mbaya na rafiki yake na kwamba yeye alishiriki zaidi katika kumshawishi kwenda katika shamba alipoikuta mauti yake na pia katika kuupoteza mwili baada ya kifo kutokea.