Saturday, March 9, 2013

Golikipa afungwa miaka 22 jela kwa kumuua mpenzi wake

Mmojawapo wa waliokuwa magolikipa bora zaidi kwenye ligi kuu ya Brazil na aliyekua nahodha wa  timu ya Flamengo ya huko inayoshiriki Ligi kuu ya Brazil juzi alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake wa zamani na kisha kuukatakata mwili wake na kuwalisha mbwa.
Bruno Fernandes de Souza alikuwa katika nafasi nzuri kuitwa kwenye timu ya taifa ya Brazil na pia kusajiliwa kwa mkataba mkubwa na timu ya AC Milan wakati siri za mauaji haya ya kutisha zilipoanza kuibuka Brazil.Alituhumiwa kumuua mpenzi wake aliyekua pia mwanamitindo nchini humo baada ya kumlaghai na kumualika katika shamba lililo katika jimbo la Minas Gerais ambako binti huyo aliuawa na kisha kukatwakatwa vipande vipande na maiti yake kulishwa mbwa waliokuwa maeneo hayo.Maiti yake haijapatikana hadi leo hii.
Mwanamitindo Eliza Samudio pichani juu aliwahi pia kutekwa siku za nyuma akiwa na ujauzito wa Bruno na kushawishiwa pamoja na kulazimishwa kuitoa mimba hiyo ambapo alikataa na kupeleka mashitaka polisi.Wakati wa kesi hiyo hakuonekana na katika uchunguzi ndo yalipoibuka haya ya mauaji ya kutisha ambapo Bruno aliwashirikisha baadhi ya ndugu zake,marafiki wa karibu,mke wake wa zamani na hata mmojawapo wa wachumba zake.
Bruno amepewa hukumu ndogo kwa sababu ya kushirikiana kwake na polisi na pia kutubu kushiriki mauaji hayo mahakamani ingawa amekua akisisitiza kwamba mrembo huyo aliuawa kwa bahati mbaya na rafiki yake na kwamba yeye alishiriki zaidi katika kumshawishi kwenda katika shamba alipoikuta mauti yake na pia katika kuupoteza mwili baada ya kifo kutokea.

No comments:

Post a Comment