Manchester United wameendeleza wimbi la ushindi na kujikita kwenye usukani wa Ligi Kuu ya Uingereza(EPL) baada ya ushindi wa goli moja lilitokana na kazi nzuri ya Robin van Persie na kumsabisha Titus Bramble wa Sunderland ajifunge kama inavyoonekana pichani juu.
Sunderland 0 - 1 Man Utd
Bramble 27 og
Manchester City leo nao hawakubaki nyuma kushikilia vizuri zaidi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kutoa adhabu kali ya magoli 4 kwa Newcastle Utd.Pichani juu Silva akifunga goli la pili.
Man City 4 - 0 Newcastle
Tevez 41
Silva 45+2
Kompany 56
Perch 69 og
Chelsea wamekutana na kisiki cha Southampton leo na wakala kipigo cha goli 2 - 1 ugenini.Pichani juu Rodriguez akimalizia mambo dhidi ya Cech.
Southampton 2 - 1 Chelsea
Rodriguez 23 John Terry 33
Rickie Lambert 35
Na the Gunnerz leo waliamka toka usingizini na kuwaweka mkiani mwa EPL timu ya Reading kwa kuwafunga magoli manne huku wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huku Kirean Gibbs akicheza mechi yake ya 100 kwa timu hiyo ya kaskazini ya London.Mnamo dakika ya saba ya mchezo uwanja wote ulisimama na kupiga makofi kama heshima ya kumbukumbu ya mchezaji namba saba wa zamani anayekumbukwa zaidi na aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa (Hodgkin's Lymphoma) mwaka 2001 maarufu kama Rocky 7 (David Rocastle)
Arsenal 4 - 1 Reading
Gervinho 11
Carzola 48
Giroud 68
Arteta 77 pen
Matokeo ya michezo mingine ni kama ifuatavyo:
Swansea 1 - 2 Tottenham
West Ham 3 - 1 West Brom
Wigan 1 - 0 Norwich
No comments:
Post a Comment