Sunday, October 7, 2012

Vettel wins at Suzuka Japanese Grand Prix

Sebastian Vettel amejipa zaidi matumaini ya kuwa bingwa wa dunia kwa mara ya tatu mfululizo katika mashindano ya magari ya langalanga (Formula 1 racing) baada ya kushinda mashindano ya magari hayo ya Japan ambapo alianza akiwa mbele na kushikilia nafasi hiyo hadi mwisho wa mashindano.Inaonekana mamekanika wa Red Bull wamekuwa kazini toka msimu uanze kutengeneza gari bora zaidi kwa ajili ya kumalizia msimu na hayo yalidhihirika katika shukrani zake kwa timu yake baada ya ushindi huo.Katika podium pia alijumuika na dereva wa Ferarri tokea Brazil Felipe Massa pamoja na mjapani Kamui Kobayashi mjapani anayeendeshea timu ya Sauber.Jenson Button alimaliza wa nne na pia Lewis Hamilton wa tano.Anayeongoza mashindano ya Dunia Fernando Alonso alipata ajali na hakumaliza mashindano baada ya kugongwa na Kimi Raikkonen.
Mark Webber dereva mwingine wa Red Bull ambae alianza mashindano akiwa mbele alimaliza wa kumi na moja baada ya kugongwa katika mzunguko wa kwanza tu na mfaransa ambaye amekuja kuwa mashuhuri kwa kugonga wenzake Roman Grosjean.
Gap kati ya Vettel na Alonso kwa sasa ni pointi 4 kukiwa kumebaki mashindano matano tu mwaka huu.


No comments:

Post a Comment