Monday, September 24, 2012

Unajua historia ya Capital One Cup?

Huu ni msimu wa 53 wa kombe hili linalojulikana pia kama kombe la ligi (The Football League Cup) na msimu uliopita tulilijua zaidi kwa jina la Carling Cup kutokana na Carling kuwa ndio wadhamini wa chama cha mpira wa miguu Uingereza mwaka huo lakini udhamini mwaka huu umehamia kwa Benki nyingine ya Capital One na kwa sababu hiyo mashindano kubadilishwa jina.Hiki ni kikombe cha pili kwa umaarufu katika michuano ya mtoano huko Uingereza ambapo mshindi huenda kucheza katika ligi ya bara la Ulaya ya Europa na ni nafasi pekee finyu kwa vilabu vichanga nchini humo kuweza kushiriki mashindano ya Ulaya hasa ukichukulia timu kubwa huwa zinachezesha timu zake za vijana na hivyo kuongeza uwezekano wa timu ndogo kushinda hii ikisababishwa na udogo wa zawadi ya mashindano haya ya pauni 100,000 kwa mshindi wa kwanza na 50,000 kwa mshindi wa pili tofauti na Kombe la FA ambalo zawadi ya kwanza huwa ni pauni mil 2.Pia ukweli kwamba timu kubwa zenye nafasi kubwa ya kushiriki UEFA Champions League na Europa League kupitia nafasi zao kwenye ligi huwa hazioni sababu ya kugombea sana kikombe hiki.
Capital One Cup inashirikisha timu 92 bora za Uingereza ambapo timu zote 92 zinashiriki katika mchezo wa mpira wa miguu ngazi ya Ligi nchini Uingereza kuanzia Ligi kuu mpaka daraja la 3 la huko.
Timu kubwa zinazoshiriki mashindano ya Ulaya huanzia hatua ya mzunguko wa tatu wakati timu zote zilizobaki huanzia raundi ya kwanza.
Mashindano haya yalianzishwa msimu wa mwaka 1960-61 na Aston Villa ndo walikuwa washindi wa mara ya kwanza.Kwa sasa bingwa mtetezi ni Liverpool walioshinda kikombe hiki msimu uliopita.Yalianzishwa hasa kama mashindano ya kati ya wiki Uingereza hasa baada ya timu nyingi kuweka taa kwenye viwanja vyake na kuongeza uwezekano wa kuchezwa kwa mechi za jioni katikati ya wiki hasa kipindi ambacho hakukuwa na mechi nyingi za katikati ya wiki za Ulaya kwa timu za Uingereza.Mzunguko wa 3 unatazamiwa kuchezwa leo na kesho ambapo timu nyingi kubwa zinatazamiwa kama kawaida kuchezesha vikosi vyao vya vijana.Mechi ngumu kabisa inatazamiwa kuwa

Manchester United   vs     Newcastle           (26/09/2012)
Manchester City       vs     Aston Villa          (25/09/2012)

Mechi nyingine zinazohusisha timu kubwa Uingereza zitakua:

25/09/2012
West Ham               vs      Wigan
Leeds Utd               vs      Everton
Chelsea                   vs      Wolves

26/09/2012
QPR                       vs      Reading
West Brom              vs      Liverpool
Carlisle                    vs      Tottenham
Arsenal                    vs     Coventry City

No comments:

Post a Comment