Sunday, September 2, 2012

Arsenal wafunga goli kwa EPL msimu huu

Pamoja na kushambuliwa sana na watangazaji na waandishi wa habari za michezo baada ya kuuzwa kwa Robin Van Persie leo Arsene Wenger alitoka uwanjani akiwa na furaha huku uwanja wa Anfield ukirindima kwa kelele za mashabiki wa Arsenal wakiimba nyimbo za furaha baada ya manunuzi ya kocha wa timu yao toka Kaskazini ya London kufanya kazi nzuri ugenini.Arsenal wameshinda mechi yao ya kwanza wakiwa wamecheza mechi 3 bila kuruhusu goli na kufikisha jumla ya pointi 5.Lukas Podolski na Santiago Carzola manunuzi ya msimu huu ya kocha Wenger ndio wachezaji walioifanya timu yao kutoka kifua mbele katika mojawapo ya viwanja vigumu kabisa kupata ushindi kwa timu ya ugenini nchini Uongereza.

No comments:

Post a Comment