Wednesday, September 26, 2012

Arsenal waanza mashindano ya Kikombe cha Ligi kwa kishindo

Hapo jana Arsenal ilianza mashindano ya Kombe La Ligi za chama cha soka cha Uingereza kwa kishindo baada ya kuishindilia timu ya Coventry City magoli 6 - 1 magoli matano ya Arsenal yakifungwa katika kipindi cha pili.Katika hali ya kutia hamasa kwa Arsenal ni mchezaji Olivier Giroud kufunga goli lake la kwanza akiwa mchezaji wa Arsenal wakati pia kulikuwa na magoli kutoka kwa Ox,Asharvin,Theo Walcott aliyefunga mawili pamoja na beki Ignasi Miquel.Goli la kufutia machozi la Coventry City lilifungwa na Callum Ball na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 6 - 1 ambapo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger  aliwachezesha zaidi wachezaji wa timu ya vijana pamoja na wale ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.Baada ya mchezo alisifia umakini wa wachezaji wake na pia kusifia kiwango chao.Arsenal imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo msimu huu ikiwa imeruhusu magoli manne tu kwenye mashindano yote.
Katika raundi ya nne inayoteazamiwa kuchezwa tarehe 29 Oktoba Arsenal itakua wageni wa Reading kushindania kuingia Robo Fainali ya mashindano haya.

No comments:

Post a Comment