Sunday, September 23, 2012

Man UTD walibebwa?

Mechi iliyosubiriwa kwa hamu hapo jana kwenye super sunday iliisha kwa mabishano mazito kuhusu uhalali wa kutolewa kadi nyekundu pamoja kutolewa kwa penati vtu viwili vilivyoifanya Manchester United kutoka kifua mbele katika mechi yao yenye upinzani mkubwa dhidi ya watani wao wa jadi Liverpool.Pamoja na kuwa ustaarabu uliotawala ulikua ni heshma tosha kwa wahanga wa ajali ya Hillsborough iliyoua watu zaidi ya 80 Liverpool kushinda ingekuwa heshima kubwa zaidi kwa wahanga hao.Kwa sehemu kubwa Liverpool pamoja na kucheza muda mwingi wa mechi wakiwa pungufu waliutawala mchezo na bahati haikuwa yao.Ni wazi kwamba wana nafasi ya kufanya vizuri katika msimu huu kwa kuangalia jinsi walivyocheza jana hasa kama wataendelea kucheza hivyo.Marudio ya kilichotokea wakati Jonjo alipopewa kadi nyekundu yanaonyesha kadi hiyo ilikuwa ni ya kionevu na kama refa wa mchezo ule angekuwa anatenda kwa haki basi angetoa pia kadi nyekundu kwa Jonny Evans na pia Robin Van Persie ambao walifanya tendo lile lile la Jonjo katika mechi hiyo.Pamoja na yote ni vigumu sana kusema wazi kwamba penati aliyotoa referee huyo ilikua si sahihi ingawa kulikuwa na mazingira ya utatanishi.Nadhani katika mazingira ya utatanishi ingekuwa vizuri kwa muamuzi kutotoa penati.
Pamoja na hayo mechi iliisha kwa ushindi wa goli 2 - 1 kwa Man Utd na hivyo kuwasogeza katika nafasi ya pili nyuma tu ya Chelsea wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 12 wakati Liverpool inaendelea kuwa nafasi ya tatu toka chini ikiwa na pointi 2 tu.

2 comments:

  1. NADHANI TUNAKOSEA KUSEMA MAN U ILIBEBWA, PIA CHUKUENI DAKIKA MOJA NA NUSU KUSEMA KWAMBA REFA ALIKOSEA. sIO MAN U ILIBEBWA!

    ReplyDelete
  2. Nadhani hili lilikua swali tu.Ila pengine ile penati ilikua uamuzi mgumu kwa refa.

    ReplyDelete