Tuesday, September 4, 2012

Zenit St.Petersburg wanaendelea na matumizi na kujiimarisha

Habari toka vyanzo mbalimbali ni kwamba Zenit St.Petersburg inayoshiriki ligi kuu ya Urusi imeendelea kujiimarisha pamoja kuwa inaongoza ligi ya Urusi na wanatazamia kushiriki ligi ya mabingwa ya UEFA(UEFA Champions League).Manunuzi ya ndani ya siku moja iliyopita ni Givanildo Vieira de Souza(miaka 26) anayejulikana pia kama Hulk kutoka Porto kwa dola milioni 50.7 na pia beki Axel Witsel(miaka 23) wa Benfica na timu ya taifa ya Ubeligiji kwa bei hiyo hiyo (wachezaji wote pichani wasaini mkataba wa miaka 5).
Hii naifanya Zenit kuwa ya tatu kwa matumizi barani ulaya na pengine duniani msimu huu nyuma ya PSG ya Ufaransa iliyotumia dola 206 millioni na Chelsea iliyotumia dola millioni 140.

No comments:

Post a Comment