Thursday, September 20, 2012

Don Vito has spoken


        Mashabiki wa Arsenal wamembatiza golikipa wao wa akiba aliyecheza mechi 3 kati ya 5 za kwanza za msimu huku akicheza mechi 2 bila kuruhusu bao jina la utani la Don Vito.Huyo ni  Vito Mannone kwa wasiomjua alitua Arsenal akitokea Atalanta ya Italia mwaka 2005 wakati huo akiwa na miaka 17 tu  na akichezea timu ya vijana ya Taifa ya Italia.Ameshakwenda kwa mkopo kupata ujuzi zaidi katika timu za Barnsley huko nyuma na Hull City msimu uliopita.Amekuwa sehemu muhimu ya timu na kuchangia kujenga ukuta thabiti akitishia kumnyang'anya jezi namba moja kipa wa kwanza aliyeumia na anayesemekana huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi mitatu ijayo Wojciech Czszecny huku golikipa namba mbili Lucasz Fabianski ameumia mgongo wakati alipokuwa na timu yake ya taifa ya Poland.
       Mannone amewataka wachezaji wenzake wa Arsenal kuhakikisha timu yao inatawala mchezo hapo Jumapili Arsenal itakapokua na mechi ya kwanza ngumu ya msimu kwani watakua wanakutana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City katika uwanja wa Etihad huko Manchester.Ikumbukwe mechi ya mwisho kati ya timu hizo Arsenal ilishinda baada ya goli zuri na pekee la mchezo toka kwa Mikel Arteta.
       Mchezaji huyo amedokeza kwamba kabla ya mechi yake ya kwanza ya msimu alikua na mazungumzo na Arsene Wenger ambapo aliambiwa kwamba amefikia kiwango na wakati wa kuipigania jezi namba moja ya timu hiyo.Tusubiri Jumapili mchana wandugu kumshuhudia golini tuweze kujua kama atatoka Etihad Stadium akishangilia au katika huzuni wakati Arsenal itakuwa ikipigania kubakia na rekodi ya kutofungwa na kutoruhusu magoli mengi ikiwa na goli moja tu la kufungwa katika ligi msimu huu.

No comments:

Post a Comment