Wednesday, September 19, 2012

Matokeo UEFA Champions League (Matchday 1)

Jumatano 19/09/2012
Group E
Fabio Quagliarella aliokoa jahazi la bibi kizee wa Turin,"Juventus" baada ya kuwasawazishia katika dakika za mwisho za mchezo wao na Chelsea kufanya matokea ya mwisho kuwa 2 - 2 ambapo magoli yalifungwa na Oscar magoli yote mawili kwa Chelsea na goli jingine la Juventus kufungwa na Vidal.
Katika mchezo mwingine wa kundi hili Shakhtar Donestk walijipatia ushindi wa mabao 2 - 0 dhdi ya Nordsjaelland na hivyo kuongoza msimamo wa kundi E baada ya mechi ya kwanza.

Group F
Katika kundi hili Bayern Munich toka Bavaria wameendeleza historia ya kufanya vizuri katika mashindano haya na msimu huu baada ya kuifunga Valencia ya Hispania magoli 2 - 1 ambapo magoli ya Bayern yalifungwa na Schweinsteiger na Kroos na lile la Valencia kufungwa na Nelson Valdez.
Hata hivyo FC BATE Borisov ndo wamejiongozea kundi hili baada ya kuwafunga LOSC Lille magoli 3-1 wakiwa ugenini na hivyo kuongoza kwa wingi wa magoli.

Group G
Lio Messi alikuwa mkombozi wa Barcelona baada ya kuwasaidia kukomboa pointi 3 katika mechi ya kwanza ya UEFA Champions league msimu huu kwa goli zake mbili za haraka haraka dakika ya 72 na ya 80.goli jingine la Barca lilifungwa na Tello.Magoli ya Spartak Moskva yalifungwa na midfielder Romulo pamoja na goli alilojifunga beki wa Barcelona Dani Alves.Matokeo ya mwisho yalikua 3 - 2.
Celtic na Benfica zilitoka suluhu ya bila kufungana hivyo Barca inaongoza kundi hili.

Group H
Goli la mapema la Michael Carrick liliwaondolea mashaka mashabiki wa Man Utd na lilikuwa tosha kabisa kuwapa pointi 3 katika uwanja wa nyumbani na hivyo kuanza kwa ushindi katika mashindano haya makubwa msimu huu.Pichani Carrick akielekea kufunga.Nani alishindwa kufunga penati katika kipindi cha pili wakati timu zote zilikosana kosana sana na Galatasaray waligongesha mwamba mara 2 na hata kusemekana kunyimwa penati mbili za wazi.

CFR Cluj wameanza vizuri mashindano haya kwa kuifunga Braga magoli 0 - 2 ambapo pia wameweza kujihakikishia kuanza kwa kuongoza kundi lao juu ya mashetani wekundu wa Manchester.







No comments:

Post a Comment