Sunday, September 2, 2012

Paralympics zaendelea London

Mashindano maalum ya riadha kwa watu wenye ulemavu mbalimbali yameendelea huko Uingereza huku kwa mara ya kwanza yakipata mahudhurio makubwa na pia kuvutia ufuatiliaji wa watu wengi zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.Mashindano haya ambayo hufuata mashindano ya Olimpiki kila yanapofanyika yameshuhudia mkimbiaji(blade runner) Oscar Pistorius wa Afrika ya Kusini aliyepata umaarufu sana kwa kushiriki mashindano ya Olimpiki akivuka vikwazo vya mapingamizi na utata mwingi akipitwa katika mbio za 200m-T44 na kumaliza wa pili.Mbrazil Alan Fonteles Cardoso Oliveira ndiye alishinda medali ya dhahabu kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment