Sunday, September 23, 2012

Hamilton Ashindwa kumaliza mashindano ya Formula 1 Singapore

Baada ya kushindwa kumaliza Singapore Grand Prix jana Lewis Hamilton ameshuka hadi nafasi ya nne katika msimamo wa ubingwa wa kuendesha magari ya kasi ya langalanga duniani ambapo pia ameongeza gepu la pointi kati yake na kinara anayeongoza mashindano hayo kwa sasa Fernando Alonso anayetokea Hispania na kuendesha magari ya Ferari.Hamilton amepitwa pia na Vettel na Raikkonen kwenye msimamo wa kugombea ubingwa wa dunia kwa sasa.Nafasi pekee aliyonayo kuwa bingwa wa dunia ni kama atashika nafasi ya kwanza au kumaliza mbele ya Alonso akibeba pointi katika mashindano 6 yaliyobakia mwaka huu kazi ambayo ni ngumu sana.Kwa sasa ameachwa pointi 52.Amekuwa na bahati mbaya mwaka huu huku makosa ya timu yake,kuharibika kwa gari na hasa gear box pamoja na ajali kumvurugia uwezekano wa kushinda ubingwa wa dunia pamoja na kuwa muendeshaji mzuri.Kumekuwa na tetesi siku za karibuni kwamba ataihama timu yake ya McLaren yenye makao yake huko Wukong China na kuhamia Mercedes ingawa amekuwa akikana.

No comments:

Post a Comment