Saturday, August 25, 2012

Lance Armstrong matatani

Bingwa mara 7 wa mashindano ya Baiskeli  ya Ufaransa yaani Tour de France bwana Lance Armstrong amejikuta matatani akiwa katika hati hati ya kupoteza mataji yake na pia kushtakiwa na hata kufungwa.Mpaka sasa heshma yake imeharibiwa na tuhuma hizi zinazomuhusisha kutumia madawa mbalimbali ya kuongeza nguvu pamoja na kutumia njia mbalimbali zisizoruhusiwa na ambazo ni kinyume na taratibu za kimashindano ambapo amehusishwa na kutumia testosterone kuharakisha uponaji wa viungo na chembehai,pia kutumia steroids kukuza misuli na kuongeza kasi ya uponaji na wakati huo huo kuongezewa damu kabla ya mashindano ili kuiongezea damu uwezo wa kubeba hewa ya Oksijeni.
Yote haya yamesemekana kupata ushahidi wa baadhi ya wanatimu wenzake na wafanyakazi wa timu yake wanaotuhumiwa naye na waliokubali kutoa ushahidi ili kupewa upendeleo maalumu katika adhabu kwa sababu ya ushirikiano wao.
USADA inayohusika na kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu michezoni huko Marekani imeshamfungia maisha na kumtangaza kumnyang'anya mataji yake ingawa Chama cha mbio za baiskeli duniani na kile cha Marekani vimepinga vikidai chama hicho hakina nguvu kisheria kufikia maamuzi hayo.

No comments:

Post a Comment