Sunday, September 30, 2012

Matokeo weekend hii Ligi kuu Ufaransa

Bordeaux wameihariba rekodi ya kutofungwa ya Lyon weekend hii

Matokeo wiki ya 7 ya ligi
Ijumaa 28/09/2012
Stade Rennais      2 - 0        LOSC Lille

Jumamosi 29/09/2012
PSG                    2 - 0         Sochaux
Ajaccio               1- 0           Stade Brestois 29
Evian                   1 - 1         Lorient
AS Nancy           0 - 2         Montpellier
OGC Nice          2 - 2          Bastia
Troyes                0 - 2          Toulouse

Jumapili 20/09/2012
Valenciennes       4 - 1          Marseille
Saint Etienne       0 - 0          Stade Reims
O. Lyonnais        0 - 2          Bordeux

Matokeo Ligi kuu Italia weekend hii(Serie A)

Pichani Diego Milito akishangilia goli lililoipa ushindi Inter dhidi ya Fiorentina waliomaliza mechi wakiwa kumi uwanjani

Matokeo wiki ya 6 ya ligi
Atalanta           1 - 5       Torino
Bologna           4 - 0       Catania
Cagliari            1 - 2       Pescara
Inter                 2 - 1      Fiorentina
Juventus           4 - 1      Roma
Lazio               2 - 1       Siena
Palermo           4 - 1       Chievo
Parma              1 - 1       Milan
Sampdoria       0 - 1       Napoli
Udinese           0 - 0       Genoa

Matokeo Ligi ya Hispania weekend hii

Pichani ni Zubicarai golikipa wa akiba wa Real Sociedad ambaye amechukua nafasi ya golikipa namba moja wa timu hiyo aliyeumia wakati wa mechi ya watani wa jadi tokea jimbo la Catalunya (The Basque Derby) kati ya timu yake na Athletic Club Bilbao


Matchday 6
Valencia            2 - 0       Zaragoza
Malaga             4 - 0       Real Betis
Real Sociedad  2 - 0       Athletic Club
Sevilla              2 - 3       Barcelona
Granada           2 - 1       Celta
Valladolid         6 - 1        Rayo Vallecano
Osasuna           4 - 0        Levante
Real Madrid     5 - 1        Deportivo
Espanyol          0 - 1        Atletico Madrid

Matokeo ya mechi Ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

Pichani Marco Reus wa Borrusia Dortmund akiwatoka mabeki wa timu yake ya zamani ya Borrusia Munchegladbach ambapo alikua chachu ya ushindi wa goli 5 - 0.

Ijumaa 28/09/2012
Dusseldorf          2 - 2 Schalke 04

Jumamosi 29/09/2012
Leverkusen        2 - 0       Greuther Furth
Bremen              0 - 2       FC Bayern
Nurenberg         0 - 2        Stuttgart
Hoffenheim        0 - 0        Augsburg
Hamburg           1 - 0        Hannover
Dortmund          5 - 0        M'gladbach

Jumapili 30/09/2012
Frankfurt           2 - 1        Freiburg
Wolfsburg         0 - 2         Mainz

Saturday, September 29, 2012

Matokeo Ligi kuu ya soka Uingereza-Matchday 6






Saturday 29/09/2012
Arsenal            1 - 2      Chelsea
Everton           3 - 1       Southampton
Fulham            1 - 2       Man City
Norwich          2 - 5       Liverpool
Reading           2 - 2       Newcastle
Stoke              2 - 0       Swansea
Sunderland      1 - 0       Wigan
Man Utd         2 - 3       Tottenham

Sunday 30/09/2012
Aston Villa      1 - 1      West Brom

Yanga yapata kocha mpya

Ernstus Wilhelmus Johannes Brandts amesaini mkataba wa kuifundisha timu ya soka ya Klabu ya michezo ya Yanga (Dar-es-salaam Young Africans) ama anavyoonekana pichani.Makamu mwenyekiti Clement Sanga akielekeza jambo kuhakikisha mambo yanafanyika kwa mujibu wa taratibu.Ni Kocha wa pili kwa Yanga msimu huu na sijui kama atakaa.

Chelsea yashinda Battle of London

Kwa mara ya kwanza Arsenal wamepoteza mchezo msimu huu walipokutana na Chelsea mapema leo kwenye uwanja wa Emirates matokeo haya yakiwa ni magoli yaliyotokana na mipira ya adhabu.Arsenal walionyesha udhaifu katika kulinda dhidi ya mipira ya adhabu na pengine lilikuwa kosa kumchezesha Laurent Koscielny leo badala ya Per Metersacker.
Chelsea ambao wamezidi kujiongezea kasi ya kuuelekea ubingwa wa Ligi msimu huu walitawala zaidi nafasi ya kiungo na pengine pengo la Abou Diaby lilikuwa dhahiri kwa Arsenal.
Magoli yalifungwa na Fernando Torres na Juan Mata kwa Chelsea na lile la Arsenal kufungwa na Gervinho.Matokeo ya mwisho Arsenal 1 - 2 Chelsea.mechi nyingine za ligi ya Uingereza EPL zinaendelea kwa sasa.

Sijui wabongo mnaijua Ryder Cup?


Ryder Cup ni kikombe mashindano ya tennis yanayochezwa kila baada ya miaka miwili kati ya timu ya Marekani dhidi ya timu ya mataifa ya Ulaya na husimamiwa kwa pamoja kati ya chama cha mchezo wa golf kiprofesheno cha Marekani (PGA of America) na kile kinachosimamia mchezo huo kiprofesheno Ulaya PGA European Tour.Washiriki hupatikana kwa viwango vyao na wachache huchaguliwa na Nahodha wa kila timu.
Cha kushangaza mwaka huu kwenye mashindano haya ni uamuzi wa jana wa Nahodha wa timu ya Marekani kutomshirikisha katika hatua za Mwisho Tiger Woods ambaye siku zilizotangulia alishindwa.Na hii ni pamoja na kwamba Marekani inaongoza ikiwa na advantage ya 5-3 ambapo wana nafasi kubwa ya kushinda kikombe cha mwaka huu.Nahodha huyo Davis Love III amesema amefanya hivyo kumpumzisha baada ya siku mbili za mwanzo akielezea kiwanja wanachotumia cha Medinah Country Club,Medinah,Illinois kuwa ni kigumu na hangependa wachezaji wa timu yake kuchoka sana kwa kucheza mechi 5 katika kipindi cha mashindano hayo.Mashindano hayo yataendelea kesho baada ya mapumziko ya leo.

Lewis Hamilton kuelekea Mercedes msimu ujao

Imethibitika kwamba Lewis Hamilton ataihama timu yake ya McLaren msimu ujao na hapo jana timu hiyo imemtangaza raia wa Mexico anayeendeshea magari ya langalanga ya timu ya Sauber kwa sasa Sergio Perez kama mbadala wake msimu ujao.
Martin Whitmarsh ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu(CEO) wa McLaren Racing ametangaza jana akielezea kufurahishwa kwake na ujio wa bwana Perez kwenye timu yake msimu ujao na kusisitiza hakuna dereva aliye mkubwa kuzidi timu.

Wednesday, September 26, 2012

Kombe la Ligi Uingereza raundi ya nne

Raundi ya nne inatazamiwa kuchezwa Okatoba 29 mwaka huu ambapo mechi kubwa kabisa inatazamiwa kuwa kati ya Chelsea na Manchester United.Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:

Sunderland      vs        Middlesbrough
Swindon          vs        Aston Villa
Wigan              vs        Bradford
Leeds              vs        Southampton
Norwich          vs        Tottenham
Liverpool         vs        Swansea
Chelsea           vs        Man Utd
Reading           vs        Arsenal

Arsenal waanza mashindano ya Kikombe cha Ligi kwa kishindo

Hapo jana Arsenal ilianza mashindano ya Kombe La Ligi za chama cha soka cha Uingereza kwa kishindo baada ya kuishindilia timu ya Coventry City magoli 6 - 1 magoli matano ya Arsenal yakifungwa katika kipindi cha pili.Katika hali ya kutia hamasa kwa Arsenal ni mchezaji Olivier Giroud kufunga goli lake la kwanza akiwa mchezaji wa Arsenal wakati pia kulikuwa na magoli kutoka kwa Ox,Asharvin,Theo Walcott aliyefunga mawili pamoja na beki Ignasi Miquel.Goli la kufutia machozi la Coventry City lilifungwa na Callum Ball na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 6 - 1 ambapo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger  aliwachezesha zaidi wachezaji wa timu ya vijana pamoja na wale ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.Baada ya mchezo alisifia umakini wa wachezaji wake na pia kusifia kiwango chao.Arsenal imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo msimu huu ikiwa imeruhusu magoli manne tu kwenye mashindano yote.
Katika raundi ya nne inayoteazamiwa kuchezwa tarehe 29 Oktoba Arsenal itakua wageni wa Reading kushindania kuingia Robo Fainali ya mashindano haya.

Monday, September 24, 2012

Unajua historia ya Capital One Cup?

Huu ni msimu wa 53 wa kombe hili linalojulikana pia kama kombe la ligi (The Football League Cup) na msimu uliopita tulilijua zaidi kwa jina la Carling Cup kutokana na Carling kuwa ndio wadhamini wa chama cha mpira wa miguu Uingereza mwaka huo lakini udhamini mwaka huu umehamia kwa Benki nyingine ya Capital One na kwa sababu hiyo mashindano kubadilishwa jina.Hiki ni kikombe cha pili kwa umaarufu katika michuano ya mtoano huko Uingereza ambapo mshindi huenda kucheza katika ligi ya bara la Ulaya ya Europa na ni nafasi pekee finyu kwa vilabu vichanga nchini humo kuweza kushiriki mashindano ya Ulaya hasa ukichukulia timu kubwa huwa zinachezesha timu zake za vijana na hivyo kuongeza uwezekano wa timu ndogo kushinda hii ikisababishwa na udogo wa zawadi ya mashindano haya ya pauni 100,000 kwa mshindi wa kwanza na 50,000 kwa mshindi wa pili tofauti na Kombe la FA ambalo zawadi ya kwanza huwa ni pauni mil 2.Pia ukweli kwamba timu kubwa zenye nafasi kubwa ya kushiriki UEFA Champions League na Europa League kupitia nafasi zao kwenye ligi huwa hazioni sababu ya kugombea sana kikombe hiki.
Capital One Cup inashirikisha timu 92 bora za Uingereza ambapo timu zote 92 zinashiriki katika mchezo wa mpira wa miguu ngazi ya Ligi nchini Uingereza kuanzia Ligi kuu mpaka daraja la 3 la huko.
Timu kubwa zinazoshiriki mashindano ya Ulaya huanzia hatua ya mzunguko wa tatu wakati timu zote zilizobaki huanzia raundi ya kwanza.
Mashindano haya yalianzishwa msimu wa mwaka 1960-61 na Aston Villa ndo walikuwa washindi wa mara ya kwanza.Kwa sasa bingwa mtetezi ni Liverpool walioshinda kikombe hiki msimu uliopita.Yalianzishwa hasa kama mashindano ya kati ya wiki Uingereza hasa baada ya timu nyingi kuweka taa kwenye viwanja vyake na kuongeza uwezekano wa kuchezwa kwa mechi za jioni katikati ya wiki hasa kipindi ambacho hakukuwa na mechi nyingi za katikati ya wiki za Ulaya kwa timu za Uingereza.Mzunguko wa 3 unatazamiwa kuchezwa leo na kesho ambapo timu nyingi kubwa zinatazamiwa kama kawaida kuchezesha vikosi vyao vya vijana.Mechi ngumu kabisa inatazamiwa kuwa

Manchester United   vs     Newcastle           (26/09/2012)
Manchester City       vs     Aston Villa          (25/09/2012)

Mechi nyingine zinazohusisha timu kubwa Uingereza zitakua:

25/09/2012
West Ham               vs      Wigan
Leeds Utd               vs      Everton
Chelsea                   vs      Wolves

26/09/2012
QPR                       vs      Reading
West Brom              vs      Liverpool
Carlisle                    vs      Tottenham
Arsenal                    vs     Coventry City

Sunday, September 23, 2012

Hamilton Ashindwa kumaliza mashindano ya Formula 1 Singapore

Baada ya kushindwa kumaliza Singapore Grand Prix jana Lewis Hamilton ameshuka hadi nafasi ya nne katika msimamo wa ubingwa wa kuendesha magari ya kasi ya langalanga duniani ambapo pia ameongeza gepu la pointi kati yake na kinara anayeongoza mashindano hayo kwa sasa Fernando Alonso anayetokea Hispania na kuendesha magari ya Ferari.Hamilton amepitwa pia na Vettel na Raikkonen kwenye msimamo wa kugombea ubingwa wa dunia kwa sasa.Nafasi pekee aliyonayo kuwa bingwa wa dunia ni kama atashika nafasi ya kwanza au kumaliza mbele ya Alonso akibeba pointi katika mashindano 6 yaliyobakia mwaka huu kazi ambayo ni ngumu sana.Kwa sasa ameachwa pointi 52.Amekuwa na bahati mbaya mwaka huu huku makosa ya timu yake,kuharibika kwa gari na hasa gear box pamoja na ajali kumvurugia uwezekano wa kushinda ubingwa wa dunia pamoja na kuwa muendeshaji mzuri.Kumekuwa na tetesi siku za karibuni kwamba ataihama timu yake ya McLaren yenye makao yake huko Wukong China na kuhamia Mercedes ingawa amekuwa akikana.

Arsenal yabeba pointi Etihad


Arsenal hapo jana imecheza mechi yake ngumu ya kwanza na matokeo ya mechi yalikuwa suluhu ya goli
1 - 1  magoli yote mawili yakifungwa na ma-centre half wa timu hizo katika mechi iliyojaa ufundi katikati ya uwanja huku kiungo wa Arsenal toka Hispania Santiago Carzola akitawala mapambano hayo.Arsenal walionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo na Arsene Wenger amesema anaamini mechi hii inaonyesha mwanga wa uwezo wa timu yake na pengine itawaongezea imani kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa msimu huu.Timu zote mbili zina mengi ya kujilaumu kwa kutoshinda mchezo wa jana lakini naamini Arsenal watajilaumu zaidi kutokana na Gervinho kupata  nafasi za wazi zaidi na kuzipoteza kizembe.Timu nyingi zimeenda Etihad na kutoka vichwa chini na kwa Arsenal kuchukua pointi ni matokeo mazuri sana kwao.Arsenal imeendeleza rekodi yake nzuri katika ulinzi ya kutofungwa msimu huu na pia imeruhusu magoli mawili tu msimu huu.
Katika mechi zingine kwenye ligi ya Uingereza weekend iliyopita matokeo yalikuwa.

Jumamosi 22/09/2012
Chelsea 1 - 0 Stoke
Southampton 4 - 1 Aston Villa
West Brom 1 - 0 Reading
West Ham 1 - 1 Sunderland
Wigan 1 - 2 Fulham
Swansea 0 - 3 Everton

Jumapili 23/09/2012

Tottenham 2 - 1 QPR
Newcastle 1 - 0 Norwich
Liverpool 1 - 2 Man Utd


Man UTD walibebwa?

Mechi iliyosubiriwa kwa hamu hapo jana kwenye super sunday iliisha kwa mabishano mazito kuhusu uhalali wa kutolewa kadi nyekundu pamoja kutolewa kwa penati vtu viwili vilivyoifanya Manchester United kutoka kifua mbele katika mechi yao yenye upinzani mkubwa dhidi ya watani wao wa jadi Liverpool.Pamoja na kuwa ustaarabu uliotawala ulikua ni heshma tosha kwa wahanga wa ajali ya Hillsborough iliyoua watu zaidi ya 80 Liverpool kushinda ingekuwa heshima kubwa zaidi kwa wahanga hao.Kwa sehemu kubwa Liverpool pamoja na kucheza muda mwingi wa mechi wakiwa pungufu waliutawala mchezo na bahati haikuwa yao.Ni wazi kwamba wana nafasi ya kufanya vizuri katika msimu huu kwa kuangalia jinsi walivyocheza jana hasa kama wataendelea kucheza hivyo.Marudio ya kilichotokea wakati Jonjo alipopewa kadi nyekundu yanaonyesha kadi hiyo ilikuwa ni ya kionevu na kama refa wa mchezo ule angekuwa anatenda kwa haki basi angetoa pia kadi nyekundu kwa Jonny Evans na pia Robin Van Persie ambao walifanya tendo lile lile la Jonjo katika mechi hiyo.Pamoja na yote ni vigumu sana kusema wazi kwamba penati aliyotoa referee huyo ilikua si sahihi ingawa kulikuwa na mazingira ya utatanishi.Nadhani katika mazingira ya utatanishi ingekuwa vizuri kwa muamuzi kutotoa penati.
Pamoja na hayo mechi iliisha kwa ushindi wa goli 2 - 1 kwa Man Utd na hivyo kuwasogeza katika nafasi ya pili nyuma tu ya Chelsea wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 12 wakati Liverpool inaendelea kuwa nafasi ya tatu toka chini ikiwa na pointi 2 tu.

Super Sunday-Manchester City vs Arsenal

Mara ya Mwisho Arsenal kwenda Etihad ni Manchester City ndo waliibuka na ushindi wa goli 1 - 0 na goli lilifungwa na kiungo mahiri wa Manchester City David Silva katika dakika ya 53.Hii ilikua Desemba mwaka jana wakati Arsenal ikisemekana kuwa na wakati mgumu baada ya kuanza msimu uliopita vibaya na ilicheza chini ya kiwango huku ikishindwa kukaa na mpira na kucheza pasi nyingi za karibu na ndefu kama ilivyo kawaida ya timu hiyo ya London.Lakini msimu mmoja baadae Arsenal inajigamba kuwa timu ya ulinzi bora msimu huu Uingereza na pengine Ulaya nzima ikiwa imeruhusu goli moja tu,rekodi ambayo haijafikiwa na timu yoyote katika madaraja yote manne ya ligi za mpira katika Taifa la Uingereza.
Manchester City wakiwa wenyeji,mabingwa watetezi na pia wakiwa na kumbukumbu ya kipigo walichokipata Emirates mwishoni mwa msimu uliopita naamini watataka kurudisha heshima leo wakiwa nyumbani kwao pamoja na kuanza vibaya mechi za klabu bingwa Ulaya kwa kufungwa na Barcelona katikati ya wiki.Pamoja na kufungwa walionyesha kiwango bora kwa kuweza kucheza kwa upinzani mkubwa dhidi ya Real Madrid.
Hakuna shabiki wa Arsenal leo asiyetaka kuimba nyimbo za kuwakejeli Samir Nasri,Gael Clichy na hata Kolo Toure baada ya ushindi katika mechi hiyo itakayoanza saa 12 kamili kwa saa za Afrika mashariki.
Tuache maneno tusubiri muda wa game wandugu.

Saturday, September 22, 2012

Super Sunday imewadia-Liverpool vs Manchester United

Nadhani wadau hakuna siku ambayo washabiki wa mpira duniani watakua makini kufuatilia mpira na kutopepesuka katika kuangalia kama leo.Na nadhani hakuna mahali duniani ambapo kuna mechi zenye mvuto na zinazoweza kuvuta hisia za watu kama mechi itakayochezwa leo kule Anfield kati ya Liverpool ambao ni wenyeji dhidi ya Manchester United ambao ni wapinzani wao wa jadi kwa miaka mingi.Upinzani wa jadi unaohusishwa na malumbano pamoja na utani kuhusu mafanikio kati ya timu hizo unaosemekana kuchochewa sana na mashabiki wa Liverpool kujigamba sana kuhusu mafanikio ya timu yao miaka ya 80 ambapo walikua wakifanya vizuri sana kwenye ligi ya Uingereza na pia Ulaya na hivyo kujisimika kama timu bora nchini humo na mojawapo ya miamba ya soka barani Ulaya,heshima ambazo Liverpool kwa ushahidi wa vikombe vyake wapo sahihi kujigamba nazo.
Miaka ya karibuni Manchester United wametokea kuwa na matokeo yenye tija zaidi wakibeba vikombe lukuki katika mashindano mbalimbali na kadiri siku zinavyokwenda wameweza kufuta gepu la vikombe na kuwafikia Liverpool kwa vikombe vya ligi kuu ya Uingereza,yaani kushinda mara 19 lakini bado hawajaweza kuwafikia kwa namba ya vikombe katika bara la Ulaya.Leo hii timu hizi zinakutana kukiwa ni siku maalum ya kumbukumbu kwa mashabiki wa Liverpool waliokufa huko Hillsborough mwaka 1989 wakati wa mechi ya nusu fainali ya kombe la FA kati ya Liverpool na Notingham Forest ambapo mashabiki 96 walikufa huku zaidi ya 700 wakijeruhiwa.Huu ulikua uwanja wa Sheffield Wednesday na ulitumika kama uwanja huru kwa ajili ya mechi hiyo.
Kwa miaka mingi mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakiimba nyimbo za kashfa na pia kukejeli vifo hivyo katika masihara yao kabla na wakati wa mechi dhidi ya mashabiki wa Liverpool ambao tukio hilo liliwagusa sana.Kwa leo kwenye kumbukumbu hii kumekuwa na hamasa ya pande zote kusahau tofauti zao na pia kuheshimu marehemu hao katika kumbukumbu hii huku Sir Alex Ferguson akiandika barua ya wazi kwa mashabiki wa timu yake ya Manchester United kuwasihi waonyeshe heshma kwa marehemu na wote wanaokumbukwa leo kabla ya mechi yao pale Anfield.
Steven Gerrard ambaye ni nahodha wa Liverpool amezungumzia kuwapa heshima stahili mashabiki hao katika mechi ya leo na kusisitiza uzito wa mechi hii katika ulimwengu wa soka kwa kuiweka juu zaidi ya mechi ya Classico ya Hispania katika mazungumzo na waandishi wa habari katika maandalizi ya mechi hii.
Timu hizi zilitoka sare ya 1 - 1 mara ya mwisho kukutana Anfield Oktoba tarehe 15 mwaka jana na magoli yalifungwa na  Steven Gerrard na Javi Hernandez.Katika mechi kumi zilizopita kati yao Liverpool wameshinda mara 4 wakati Man Utd wameshinda mara 5 na kutoka suluhu mara 1.Ndani ya masaa 6 yajayo joto likipanda macho yetu wote yatakuwa Anfield kufuatilia pambano hili.May the best team win.

Thursday, September 20, 2012

Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza EPL(Matchday 5)

Jumamosi 22/09/2012

2:45pm     Swansea           vs       Everton
5:00pm     Chelsea            vs       Stoke
   "             Southampton   vs       Aston Villa
   "             West Brom      vs       Reading
   "             West Ham       vs       Sunderland
   "             Wigan              vs       Fulham


Jumapili 23/09/2012
  
3:30pm     Liverpool        vs       Man Utd
5:00pm     Newcastle       vs       Norwich
6:00pm     Man City        vs        Arsenal
   "            Tottenham       vs        QPR


Mayweather vs Manny Pacquiao pengine mwakani?!!

Baada ya Manny Pacquiao kukubali masharti ya Mayweather kwenye mgawanyo wa pesa mabingwa hawa wa kihistoria huenda wakapigana mwakani na kumaliza ubishi wa muda mrefu kwamba nani ni zaidi kati yao.Mayweather ameachiwa toka gerezani mwezi uliopita na amekua mkimya sana na Pacman anajiandaa na pambano la kukata na shoka Dec 8 dhidi ya bingwa mpya wa dunia Marquez ambapo atakua anapigana na Marquez kwa mara ya nne ingawa huko nyuma kumekua na utata kuhusu waamuzi waliotumika na uhalali wa matokeo wa mapambano kati yao.Iwapo Pacquiao atashinda itaongeza hamasa la pambano kati yake na Mayweather.Pacman amekubali mgawanyo wa malipo kati yao kuwa asilimia 55 kwa asilimia 45 kama alivyotaka Maywether mwanzoni.

Don Vito has spoken


        Mashabiki wa Arsenal wamembatiza golikipa wao wa akiba aliyecheza mechi 3 kati ya 5 za kwanza za msimu huku akicheza mechi 2 bila kuruhusu bao jina la utani la Don Vito.Huyo ni  Vito Mannone kwa wasiomjua alitua Arsenal akitokea Atalanta ya Italia mwaka 2005 wakati huo akiwa na miaka 17 tu  na akichezea timu ya vijana ya Taifa ya Italia.Ameshakwenda kwa mkopo kupata ujuzi zaidi katika timu za Barnsley huko nyuma na Hull City msimu uliopita.Amekuwa sehemu muhimu ya timu na kuchangia kujenga ukuta thabiti akitishia kumnyang'anya jezi namba moja kipa wa kwanza aliyeumia na anayesemekana huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi mitatu ijayo Wojciech Czszecny huku golikipa namba mbili Lucasz Fabianski ameumia mgongo wakati alipokuwa na timu yake ya taifa ya Poland.
       Mannone amewataka wachezaji wenzake wa Arsenal kuhakikisha timu yao inatawala mchezo hapo Jumapili Arsenal itakapokua na mechi ya kwanza ngumu ya msimu kwani watakua wanakutana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City katika uwanja wa Etihad huko Manchester.Ikumbukwe mechi ya mwisho kati ya timu hizo Arsenal ilishinda baada ya goli zuri na pekee la mchezo toka kwa Mikel Arteta.
       Mchezaji huyo amedokeza kwamba kabla ya mechi yake ya kwanza ya msimu alikua na mazungumzo na Arsene Wenger ambapo aliambiwa kwamba amefikia kiwango na wakati wa kuipigania jezi namba moja ya timu hiyo.Tusubiri Jumapili mchana wandugu kumshuhudia golini tuweze kujua kama atatoka Etihad Stadium akishangilia au katika huzuni wakati Arsenal itakuwa ikipigania kubakia na rekodi ya kutofungwa na kutoruhusu magoli mengi ikiwa na goli moja tu la kufungwa katika ligi msimu huu.

Wednesday, September 19, 2012

Matokeo UEFA Champions League (Matchday 1)

Jumatano 19/09/2012
Group E
Fabio Quagliarella aliokoa jahazi la bibi kizee wa Turin,"Juventus" baada ya kuwasawazishia katika dakika za mwisho za mchezo wao na Chelsea kufanya matokea ya mwisho kuwa 2 - 2 ambapo magoli yalifungwa na Oscar magoli yote mawili kwa Chelsea na goli jingine la Juventus kufungwa na Vidal.
Katika mchezo mwingine wa kundi hili Shakhtar Donestk walijipatia ushindi wa mabao 2 - 0 dhdi ya Nordsjaelland na hivyo kuongoza msimamo wa kundi E baada ya mechi ya kwanza.

Group F
Katika kundi hili Bayern Munich toka Bavaria wameendeleza historia ya kufanya vizuri katika mashindano haya na msimu huu baada ya kuifunga Valencia ya Hispania magoli 2 - 1 ambapo magoli ya Bayern yalifungwa na Schweinsteiger na Kroos na lile la Valencia kufungwa na Nelson Valdez.
Hata hivyo FC BATE Borisov ndo wamejiongozea kundi hili baada ya kuwafunga LOSC Lille magoli 3-1 wakiwa ugenini na hivyo kuongoza kwa wingi wa magoli.

Group G
Lio Messi alikuwa mkombozi wa Barcelona baada ya kuwasaidia kukomboa pointi 3 katika mechi ya kwanza ya UEFA Champions league msimu huu kwa goli zake mbili za haraka haraka dakika ya 72 na ya 80.goli jingine la Barca lilifungwa na Tello.Magoli ya Spartak Moskva yalifungwa na midfielder Romulo pamoja na goli alilojifunga beki wa Barcelona Dani Alves.Matokeo ya mwisho yalikua 3 - 2.
Celtic na Benfica zilitoka suluhu ya bila kufungana hivyo Barca inaongoza kundi hili.

Group H
Goli la mapema la Michael Carrick liliwaondolea mashaka mashabiki wa Man Utd na lilikuwa tosha kabisa kuwapa pointi 3 katika uwanja wa nyumbani na hivyo kuanza kwa ushindi katika mashindano haya makubwa msimu huu.Pichani Carrick akielekea kufunga.Nani alishindwa kufunga penati katika kipindi cha pili wakati timu zote zilikosana kosana sana na Galatasaray waligongesha mwamba mara 2 na hata kusemekana kunyimwa penati mbili za wazi.

CFR Cluj wameanza vizuri mashindano haya kwa kuifunga Braga magoli 0 - 2 ambapo pia wameweza kujihakikishia kuanza kwa kuongoza kundi lao juu ya mashetani wekundu wa Manchester.







Matokeo Ligi kuu ya Tanzania Bara (Matchday 2)





JKT Ruvu          0 - 2      Simba
Ruvu Shooting   2 - 1      JKT Mgambo
Prisons              1 - 1      Coastal Union
African Lyon     1 - 0       Polisi Moro
Kagera Sugar   1 - 1        JKT Oljoro
Toto Africa       2 -  2      Azam FC
Mtibwa Sugar   3 - 0       Yanga

Tuesday, September 18, 2012

Matokeo UEFA Champions League(Matchday 1)

Jumanne 18/09/2012


Magoli toka kwa Lucho Gonzalez na Steven Defour yameihakikishia Porto ushindi wa goli 2 - 0 dhidi ya Dinamo Zagreb.Dinamo wameendelea kupoteza mechi za makundi katika mashindano haya baada ya kutopata hata pointi moja toka kwenye kundi lao msimu uliopita.


PSG wameanza vizuri mashindano haya hatua ya makundi baada ya kuwaliza Dynamo Kyiv magoli 4 - 1.Magoli ya PSG waliokua nyumbani yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic (pen),Thiago Silva,Alex na la mwisho Javier Pastore.Bao la kufutia machozi la Dynamo lilifungwa na Miguel Veloso.


Arsenal wameanza vizuri msimu huu na kufikia mechi tano bila kufungwa huku wakipata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Montpellier ugenini.Magoli ya Arsenal yalifungwa na Lucas Podolski pamoja na Gervinho wakati lile la Montpeller lilifungwa na Younes Belhada.


Malaga walikua washindi dhidi ya Zenit St.Petersburg kwa magoli 3 - 0 toka kwa Isco magoli mawili na pia mkogwe Javier Saviola alijipatia bao moja.


Baada ya kuanza vibaya ligi ya Italia (Serie A) jana AC Milan walianza na suluhu ya bila kufungana dhidi ya Anderletch.Milan walikua nyumbani.


Borrusia Dortmund ambao ni mabingwa wa zamani wa kombe hili walianzia vizuri uwanja wa nyumbani kwa ushindi wa goli lililofungwa na Robert Lewandowski dhidi ya Ajax.Katika mechi ya kundi D.Naamini ni kundi gumu zaidi msimu huu.


Real Madrid ambao ni mabingwa wa kihistoria wa kombe la mabingwa la UEFA jana walithibitisha ubabe wao walipowaliza Manchester City magoli 3-2 huku magoli matatu ya mechi hiyo yakifungwa dakika za majeruhi na kuupa mchezo huo msisimko wa kipekee.Magoli ya Real yalifungwa na Ozil,Benzema na Ronaldo na yale ya Manchester City yalifungwa na Dzeko na Kolarov.


Schalke walimaliza hadithi ya timu za kundi B kushinda ugenini na wao walipojipatia ushindi wa goli 1 - 2 wakiwafunga Olympiacos nyumbani kwao.Hii imewafanya walingane kwa kila namna na Arsenal na kuongoza kundi B pamoja.Magoli yalifungwa na Benedict Howedes na Klaas Jan Huntelaar.Goli la Olympiacos lilifungwa na Djamel Abdoun.








Monday, September 17, 2012

Wadau mnamjua Armadillo?

Najua wengi mtashangaa lakini huyu ni katuni atakayetumika kulitangaza kombe la dunia litakalochezwa Brazil mwaka 2014 (Yaani 2014 FIFA World Cup Brazil) na ametangazwa kuwa balozi wa mashindano hayo jana kama chaguo la chama cha mpira wa miguu Brazil ambao ni wenyeji kamili wa mashindano hayo kupitia TV Globo kupitia kipindi chake cha soka kinachojulikana kama Fantastico.Ronaldo de Lima aliye mmoja wa wanakamati katika kamati ya maandalizi pamoja na Jerome Valke ambaye ni katibu mkuu wa FIFA wamefurahia kutangazwa huko kwa kikaragosi huyu(mascot) kuwakilisha mashindano hayo.
Armadillo ni mnyama mwenye asili ya Brazil ambaye amekaribia kabisa kupitoe (endangered specie) na jina lake la kisayansi ni Tolypeutes tricinctus
 

Bologna wawashangaza Roma dakika za majeruhi

Roma wakijua wamefanikiwa kushinda nyumbani kwao Stadio Olimpico baada ya kuongoza kwa goli 2-0 katika dakika 16 (Alessandro Florenzi na Erik Lamella)  za mwanzo za mchezo walishuhudia wapinzania wao katika ligi kuu ya Italia Serie A Bologna wakishangilia ushindi wao wa kwanza na pointi zao za kwanza msimu huu baada ya kujipatia ushindi ndani ya dakika 18 za mwisho za mchezo.Magoli ya Bologna yalifungwa na Alberto Gilardino (72',90') na Alessandro Diamanti (73').
Katika mechi zingine za Serie A matokeo yalikua.

Chievo        1 - 3     Lazio
Fiorentina    2 - 0     Catania
Genoa         1 - 3     Juventus
Milan           0 - 1    Atalanta
Napoli         3 - 1    Parma
Palermo       1 - 1    Cagliari
Pescara        2 - 3   Sampdoria
Siena            2 - 2   Udinese
Torino          0 - 2    Inter

UEFA Champions League(Matchday 1)

Jumanne 18/09/2012 saa 10:30 pm (EAT)
Dinamo                    vs          Dynamo Kyiv
Montpellier               vs         Arsenal
Malaga                     vs         Zenit St.Petersburg
Milan                        vs         Anderletch
Dortmund                 vs         Ajax
Real Madrid             vs         Man City
Olympiacos              vs          Schalke

Jumatano 19/09/2012 saa 10:30 pm (EAT)
Chelsea                     vs         Juventus
Celtic                        vs         Benfica
Man Utd                   vs         Galatasary
Braga                        vs         CFR Cluj
LOSC                       vs         BATE
Bayern                       vs        Valencia
Barcelona                  vs         Spartak Moskva
Shakhtar Donetsk      vs         Nordsjaeland

Sunday, September 16, 2012

Arsene Wenger atangazwa kocha mpya Arsenal-Miaka 16 iliyopita

Miaka 16 iliyopita tarehe kama ya leo alitangazwa rasmi kama kocha wa timu ya Arsenal akitokea katika ligi ya Japan yaani J-league na waandishi wengi wa habari wa Uingereza kumbeza wakidai ametoka kwenye ligi dhaifu na isiyojulikana na kwamba yeye mwenyewe hakua akijulikana.Amekua kocha wa pili kwa mafanikio Uingereza katika kipindi chote hicho huku akiwa na pesa finyu za kufanya mabadiliko katika timu.

Matokeo Ligi kuu Uingereza-EPL

Jumamosi 15/09/2012

Norwich       0 - 0     West Ham Utd
Arsenal         6 - 1     Southampton
Aston Villa    2 - 0     Swansea
Fulham         3 - 0     West Brom
Man Utd      4 - 0     Wigan
QPR            0 - 0     Chelsea
Stoke           1 - 1     Man City
Sunderland   1 - 1     Liverpool

Matokeo ya ligi kuu Tanzania Bara

Jumamosi tarehe 15/09/2012

Simba                   3 - 0      African Lyon
Ruvu Shooting      1 - 2      Ruvu JKT
Coastal Union      1 - 0      Mgambo JKT
Prison FC            0 - 0      Yanga SC
Kagera Sugar      0 - 1       Azam FC
Toto African        1 - 1       JKT Oljoro
Polisi Moro         0 - 0       Mtibwa Sugar

Friday, September 14, 2012

QPR vs Chelsea kupeana mikono kama kawaida

Kutakua na kupeana mikono kati ya wachezaji wa timu hizi mbili kesho katika mechi yao inayotazamiwa kuanza saa 11 jioni kwa saa za Afrika mashariki.Ikumbukwe kuna ugomvi mkubwa baina ya mabeki wa timu hizi mbili Anton Ferdinand na John Terry ambapo Terry anatuhumiwa kutumia lugha ya kibaguzi wakati timu hizo zilipopambana msimu uliopita.Je watachuniana?Maana wote wapo fiti kwa mechi hapo kesho na wana nafasi kubwa ya kucheza.

Julio Cesar Chavez jr vs Sergio Martinez kugombea ubingwa wa Dunia Middleweight kesho

Kwa kweli hutaki kuwakosa wababe hawa wakigombea ubingwa wa dunia wa middleweight ambapo Chavez jr ni WBC middleweight champion na Martinez ni WBC Diamond middleweight champion.Ni pambano linalosubiriwa kwa hamu na litaanza saa 10 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki wakati kule Marekani itakuwa jioni saa 3 ya Jumamosi tarehe 15.Pengine nitarusha link ya hili pambano tukae mkao wa kula.

Ratiba Ligi kuu Hispania-La Liga(Matchday 4)

Jumamosi 15/09/2012
Malaga                vs       Levante
Valencia               vs       Celta Vigo
Getafe                  vs      Barcelona
Sevilla                  vs      Real Madrid

Jumapili 16/09/2012
Espanyol             vs       AthleticClub
Granada              vs       Deportivo
Osasuna              vs       Mallorca
Real Sociedad     vs       Zaragoza
Atletico Madrid   vs       Rayo Vallecano

Jumatatu 17/09/2012
Valladolid            vs       Real Betis


Ratiba ya wiki hii Ligi kuu Uingereza-EPL

Jumamosi 15/09/2012
Saa 8:45   mchana      Norwich     vs      West Ham Utd
Saa 11:00   jioni         Arsenal       vs      Southampton
       "             "           Aston Villa  vs      Swansea
       "             "           Fulham        vs     West Brom
       "             "           Man Utd     vs     Wigan
       "             "           QPR           vs     Chelsea
       "             "           Stoke          vs     Man City
Saa 1:30  usiku          Sunderland  vs     Liverpool

Jumapili 16/09/2012
Saa 12:00 jioni          Reading      vs     Tottenham

Jumatatu 17/09/2012
Saa 4:00  usiku         Everton       vs    Newcastle          

Ligi kuu ya soka ya Vodacom-Tanzania Bara ratiba(Matchday 1)

Mechi za ufunguzi tarehe 15/09/2012

Simba                   vs        African Lyona           Uwanja wa Taifa     Dar-es-salaam.
Polisi Moro           vs        Mtibwa Sugar          Jamhuri                   Morogoro.
Tanzania Prisons    vs       Young Africans         Sokoine                  Mbeya
Mgambo JKT       vs        Coastal Union          Mkwakwani            Tanga
JKT Ruvu             vs        Ruvu Shootings        Azam Complex       Dar-es-salaam
Kagera Sugar       vs        Azam FC                 Kaitaba Stadium      Kagera
Toto Africans        vs       JKT Oljoro             CCM Kirumba        Mwanza

Tuesday, September 11, 2012

Simba SC yabeba kombe la hisani

Simba ya Dar-es-salaam ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom hapo jana imeanza msimu mpya kwa kunyakua kikombee cha kwanza cha msimu ilipoifunga Azam FC aliyekuwa mshindi wa pili katika mechi ya kombe la hisani inayoashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara ya Vodacom.Simba ilishinda magoli 3-2 dhidi ya wanalambalamba na kukataa uteja.

Mbuyu Twite na Yondani ruksa kuchezea Yanga

Baada ya kamati ya sheria,maadili na hadhi ya wachezaji kuridhia usajili wa wachezaji hawa wawili kuwa halali wamepitishwa rasmi kuichezea Yanga kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara,Vodacom Premier League inayotarajiwa kuanza siku ya jumamosi tarehe 15/09/2012.Kwa usajili ya Mbuyu Yanga inatakiwa kuilipa Simba dola 32,000 inazosemekana Wekundu wa Msimbazi walimpatia mchezaji huyo huko Kigali.Wachezaji hawa kwenda Yanga kumewaumiza sana mahasimu wao Simba baada ya Twite kuwabeza na Yondani kuhamia Yanga akitokea Simba.

Monday, September 10, 2012

Andy Murray ashinda Granda Slam ya kwanza

Andy Murray ameshinda mashindano makubwa (Grand Slam) kwa mara ya kwanza katika maisha yake usiku wa kuamkia leo kwenye mashindano ya Wazi ya Marekani (US Open) hii ikiwa ni mara ya tano kwake kucheza fainali kwenye Grand Slam.Kati ya mashabiki waliokuwa uwanjani ni Muigizaji maarufu aliyewahi kuigiza kama James Bond bwana Sean Connery na kocha wa Manchester United Alex Ferguson waliokuwa wakimshabikia.Fainali hii alikutano na Novac Djokovic wa Serbia huko New York kwa seti 7-6,7-5,2-6,3-6,6-2.Serena Williams alishinda mashindano hayo kwa wanawake jana ikiwa mara yake ya nne kufanya hivyo.

Sunday, September 9, 2012

Lewis Hamilton mshindi pale Monza(Italian GP)

Lewis Hamilton raia wa Uingereza na dereva wa McLaren masaa machache yaliyopita ameionyesha dunia uwezo wake mkubwa baada ya kuongoza Formula 1 Italian Grand Prix kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mashindano na kushinda mashindano hayo akipanda mpaka nafasi ya 2 katika kuwania ubingwa wa dunia mwaka huu akiwa nyuma ya Fernando Alonso ambaye ni Raia wa Hispania na dereva wa Ferari kwa pointi 37 tu.Alonso alimaliza wa tatu katika mashindano hayo.