Friday, August 31, 2012

Atletico de Madrid washinda European Super Cup

Hat-trick ya kipindi cha kwanza ya Radamel Falcao pamoja na nyongeza ya bao moja lililofungwa na Miranda kipindi cha pili yalitosha kuwapa ushindi wa goli 4-1 Atletico de Madrid dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stade Louis II dakika chache zilizopita.Kwa maana hii Atletico wataliwakilisha bara la Ulaya katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia katika msimu huu.Chelsea ilijipatia bao la kufutia machozi dakika ya 75 kupitia kwa Gary Cahill.

Thursday, August 30, 2012

Michael Schumacker kushiriki Grand Prix ya 300

Michael Schumacker atashiriki mashindano ya 300 ya magari ya langa langa (Formula One Racing) siku ya jumapili katika mzunguko au circuit anayoiita sebuleni kwake kwani Belgian Grand Prix itafanyikia kwenye uwanja wa Spa ambapo mwendesha magari huyu bingwa mara saba wa dunia aliendesha kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1991 na pia ambapo alishinda kwa mara ya kwanza pia mwaka uliofuata.Wakati akishiriki Mwingereza Lewis Hamilton mwenye pointi 117 atakua anapambana kupata ushindi na kupunguza gap la point na anayeongoza mashindano ya dunia mwaka huu huku kukiwa na mabishano ndani ya timu ya McLaren baada ya mwingereza mwenzake Jenson Button(pointi 76) mwenye nafasi finyu ya kupata ubingwa wa dunia mwaka huu kutamka kwamba hatamsaidia mwenzake kufanya vyema zaidi kwenye mashindano ya kuwania ubingwa wa dunia mwaka huu.Fernando Alonso anaongoza mashindano ya kuwania ubingwa wa dunia akiwa na pointi 164

UEFA Super cup leo Usiku (Chelsea vs Atletico Madrid)

Hii inatazamiwa kuwa leo usiku pale Stade de Louis II,mjini Monaco ambapo Chelsea ambao ni mabingwa wa Kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) watakabana koo na Atletico Madrid ambao ni mabingwa wa Kombe la Europa League.Mshindi wa mechi hii huwa anapata nafasi ya kuliwakilisha bara la Ulaya kwenye mashindano ya klabu bingwa duniani.
Mechi itaanza kuchezwa saa 2 na dakika 45 kwa saa za Monaco.Hii itakua saa 3 na dakika 45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki

Makundi ya UEFA Champions League 2012/2013






Group A: Porto, Dynamo Kiev, PSG, Dinamo Zagreb
Group B: Arsenal, Schalke, Olympiakos, Montpellier
Group C: AC Milan, Zenit, Anderlecht, Malaga
Group D: Real Madrid, Man City, Ajax, Dortmund
Group E: Chelsea, Shakhtar, Juventus, Nordsjaelland
Group F: Bayern, Valencia, Lille, BATE
Group G: Barcelona, Benfica, Spartak Moscow, Celtic
Group H: Man Utd, Braga, Galatasaray, Cluj.

Iniesta mchezaj bora Ulaya

Andreas Iniesta ametangazwa jana kuwa mchezaji bora wa mwaka Ulaya baada ya kupigiwa kura kuwa bora zaidi katika bara hilo na waandishi wa habari za michezo toka nchi wanachama wa chama cha mpira barani Ulaya (UEFA).Kiungo huyo wa timu ya soka ya Barcelona na pia tima ya soka ya taifa ya Hispania ameshinda kombe la dunia pamoja na lile la Ulaya akiwa na timu yake ya taifa ambapo mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya lililopita liliisha akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano baada ya kucheza mechi zote ilizoshiriki timu yake.Iniesta pia ana rekodi ya kucheza zaidi ya mechi 50 za La Liga mfululizo bila timu yake kufungwa.Mchezaji huyo aliwashukuru wachezaji wenzake wa timu zote mbili na kuwakaribisha kushiriki tuzo yake hiyo.

Wednesday, August 29, 2012

Mbuyu Twite kuwasili leo

Habari rasmi zenye uthibitisho wa uongozi wa Young Africans SC ni kwamba Mbuyu Twite ambaye ni beki raia wa Rwanda mwenye asili ya DRC atawasili leo na kujiunga na wenzake kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Coastal Union siku ya Jumamosi.Mchezaji huyu anatazamiwa kupata mapokezi makubwa hasa ukichukuliwa usajili wake uligubikwa na mashindano makubwa kati ya Yanga na wapinzani wao wakubwa Simba.

Real Madrid washinda Spanish Super Cup

Hatimaye Real Madrid wameshinda Spanish Super Cup kikiwa ni kikombe cha kwanza mzimu huu huko Hispania.Hiyo ilikuwa ni baada ya kushinda mchezo wa marudiano Santiago Bernabeu kwa magoli 2-1.Mchezo wa kwanza uliochezwa Nou Camp uliisha kwa matokeo ya 3-2 na hivyo Madrid inashinda kombe hilo kwa kufunga magoli mengi ya ugenini.Pongezi nyingi kwa Real Madrid

Monday, August 27, 2012

Luka Modric atua Santiago Bernabeu

Mtandao wa Klabu ya Real Madrid umetangaza rasmi uhamisho wa Luka Modric toka Tottenham Hotspurs ya Kaskazini ya London na inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza na kujiunga na weupe hao wa Madrid.

Sunday, August 26, 2012

JAVIER ZANETTI

Leo bwana mkubwa huyu tokea Argentina ameweka historia kwa kuichezea timu yake ya Inter Milan mechi ya 800.Nadhani ni rekodi duniani ila kama kuna mwenye rekodi ya mtu mwingine kucheza mechi nyingi zaidi atuambie."Sijui kama nimeshaangalia mechi 800 maishani mwangu-Andrea Stramaccioni"

Madrid waumizwa na jirani zao Getafe

Real Madrid wameaibishwa na jirani zao Getafe katika mechi yao ya pili ya msimu mpya wa La Liga huku ikiwa ni mechi ya pili mfululizo kupoteza baada ya kufungwa na Barcelona katikati ya wiki katika mcheza wa kugombea Spanish Supercup.Getafe wameibuka na ushindi wa magoli 2-1 na kuwaweka pabaya Real Madrid katika harakati zao za kutetea ubingwa wa La Liga ambapo hadi sasa wameachwa pointi 5 na Barcelona ambao wamekuwa wapinzani wao wakubwa katika kugombea kombe hilo siku za karibuni.

Saturday, August 25, 2012

Lance Armstrong matatani

Bingwa mara 7 wa mashindano ya Baiskeli  ya Ufaransa yaani Tour de France bwana Lance Armstrong amejikuta matatani akiwa katika hati hati ya kupoteza mataji yake na pia kushtakiwa na hata kufungwa.Mpaka sasa heshma yake imeharibiwa na tuhuma hizi zinazomuhusisha kutumia madawa mbalimbali ya kuongeza nguvu pamoja na kutumia njia mbalimbali zisizoruhusiwa na ambazo ni kinyume na taratibu za kimashindano ambapo amehusishwa na kutumia testosterone kuharakisha uponaji wa viungo na chembehai,pia kutumia steroids kukuza misuli na kuongeza kasi ya uponaji na wakati huo huo kuongezewa damu kabla ya mashindano ili kuiongezea damu uwezo wa kubeba hewa ya Oksijeni.
Yote haya yamesemekana kupata ushahidi wa baadhi ya wanatimu wenzake na wafanyakazi wa timu yake wanaotuhumiwa naye na waliokubali kutoa ushahidi ili kupewa upendeleo maalumu katika adhabu kwa sababu ya ushirikiano wao.
USADA inayohusika na kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu michezoni huko Marekani imeshamfungia maisha na kumtangaza kumnyang'anya mataji yake ingawa Chama cha mbio za baiskeli duniani na kile cha Marekani vimepinga vikidai chama hicho hakina nguvu kisheria kufikia maamuzi hayo.

Ligi kuu ya Soka Italia yaanza

Ligi kuu ya Italia imeanza wiki hii huku ikigubikwa na utata baada ya ushindi wa mabingwa watetezi Juventus kuanza kwa kuifunga Parma huku magoli yote mawili yakiwa na utata baada ya la Andrea Pirlo kusemekana halikuvuka mstari pamoja na kukubaliwa na refa.Mie sitaki kubisha wala kukabali.

Matokeo wiki ya kwanza ligi ya Ujerumani

24/08/2012
                                             Dortmund       2 - 1        Bremen

25/08/2012
                                 Monchengladbach      2 - 1       Hoffenheim
                                                Freiburg      1 - 1       Mainz
                                              Augsburg      0 - 2       Dusseldorf
                                               Hamburg      0 - 1       Nurenburg
                                       Greuther Furth      0 - 3       FC Bayern
                                           E. Frankfurt      2 - 1       Leverkusen
                                                Stuttgart      0 - 1       Wolfsburg

Thursday, August 23, 2012

BARCELONA vs REAL MADRID IN THE SPANISH SUPERCUP TONIGHT

Leo saa tano na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki miamba miwili ya soka ya Hispania itakuwa inaonyeshana ubabe katika kugombea Spanish Supercup ambapo mechi ya kwanza itachezwa nyumbani kwa Barcelona na mechi ya marudiano siku ya jumatano tarehe 29/08/2012 itakua kule Santiago Bernabeu.
Nimeonelea niwakumbushe tu ndugu zangu na pengine nitaweka link ya kuwasaidia kuwatch game kwenye net baadae MUNGU akitujalia uzima na wasaa.

Wednesday, August 22, 2012

UMEPATA KUMSIKIA FABRICE OLINGA?!

Huyu ni kinda aliyeweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kabisa kuwahi kufunga goli katika ligi kuu ya Hispania La Liga.Kijana toka Cameroon na anayeichezea Malaga ya Hispania alifunga goli hilo la ushindi dhidi ya Celta Vigo na ni matunda ya malezi mazuri ya Samuel Eto'o Foundation ndugu zangu.Alifunga goli hilo dakika 6 kabla ya mpira kwisha na Malaga wamemtunuku kwa kumuweka kwenye listi yao ya wachezaji watakaocheza Europa League.Alifunga akiwa na umri wa miaka 16 na siku 98.

DANNY WELBECK ARIDHIA MKATABA MPYA MAN UTD

Mtandao wa Manchester United umethibitisha hivi punde kwamba Danny Welbeck ameridhia kwa maandishi mkataba mpya ambao utamuweka klabuni hapo kwa miaka minne ijayo.Hii inakuja kipindi ambapo timu hiyo ya upande mwekundu wa Manchester imemsajili Robin Van Persie toka Arsenal na pia ikisemekana kumfukuzia mshambuliaji Angelo Henrique toka Chile.Hii inaonyesha kujiamini kwa mshambuliaji huyo(Welbeck) hasa ukichukulia timu hiyo ina washambuliaji wengi wazuri na inatoa options nyingi zaidi kwenye ushambuliaji kwa timu hii ya Machester yenye vikombe 19 vya ligi  ya EPL.

Tuesday, August 21, 2012

JACK WILSHERE KUANZA MAZOEZI NDANI YA WIKI 4

Habari za kuaminika toka vyanzo mbalimbali ndani ya timu ya Arsenal vimesemekana kuthibtisha kwamba kiungo mdogo na mahiri wa timu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza Jack Wilshere ambaye alikuwa majeruhi msimu mzima uliopita baada ya kuumia katika mechi za kirafiki kabla ya msimu kuanza huenda akaanza mazoezi mazito ndani ya wiki 4 zijazo na hivyo kurudi uwanjani.Hii itasaidia sana timu hiyo yenye mafanikio zaidi katika jiji la London na itakuwa kama usajili mpya.
Tovuti ya Arsenal imethibitisha pia kwamba mchezaji huyo anatazamiwa kurudi uwanjani akiwa pamoja na wachezaji wengine wa Arsenal kama Bacary Sagna,Tomas Rosicky na pia Emmanuel Frimpong.

Monday, August 20, 2012

NBA

Habari toka Marekani ni kwamba kocha aliyepokea timu ya New Orleans Hornets wakati ikiwa kwenye wakati mgumu msimu uliopita akiiwezesha kucheza kwenye hatua ya mtoan(playoffs) katika msimu wake wa kwanza kama kocha mkuu wa timu Monty Williams ameongezewa mkataba ambapo atakuwa na Hornets kwa miaka minne mkataba wake ukiishia msimu wa 2015-2016.

Mo Farah uso kwa uso na Haile Gebrlselassie

Hii inatazamiwa kutokea huko Newcastle mwezi ujao tarehe 16 kwenye Mashindano ya Nusu Marathon ya Newcastle yanayojulikana kama Bupa Great North Run ambapo wakali hawa wanatazamiwa kukutana huku Mohamed Farah,Muingereza mwenye asili ya Somalia akitazamiwa kuwa Raia wa kwanza wa Uingereza kukimbia nusu marathoni ndani ya saa moja(Dakika 60) au pungufu hasa akiwa ndani ya ardhi ya Uingereza.Bingwa huyu wa mita 5000 na mita 10,000 kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika huko London hivi karibuni amewahi kukimbia Nusu Marathon kama mshindani mara moja tu katika mashindano ya marathon ya New York yaliyopita ambapo alishinda akitumia saa 1:00:23 atakuwa anakabiliana na Gebrsellasie mwenye rekodi bora ya dakika 58:55 na aliyeyashinda mashindano hayo kwa muda wa dakika 59:33 mwaka juzi (2010)

USAJILI ARSENAL

Habari za kuaminika zimesambaa kupitia vyombo mbali mbali vya habari vikiongelea usajili wa Arsenal ambapo inasemekana katika wiki inayokuja Arsene Wenger amejipanga kutangaza usajili wa wachezaji watatu wa kukata na shoka.Wachezaji hao ni Nuri Sahin anayechukuliwa kwa mkopo toka Real Madrid huku habari zikidai mkopo umepita na unasubiri tu kutangazwa.

Wakati huo huo kiungo mkabaji wa Renne ya Ufaransa pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa Yann M'villa anasemeka kuwa atafika London wiki hii kwa ajili ya uchunguzi wa afya na makubaliano ya Mwisho na Gunners.

Pia huko Hispania Fernando Llorente hakucheza mechi ya ufunguzi wa ligi ya huko kwa timu yake ya Athletic Bilbao na anasemekana kuwa katika mlango wa kuhama akihusishwa pia na kutua Emirates wiki ijayo.

Timu ya AC Milan inasemekana kuongeza kasi yake katika kumhamishia Arsenal beki wake wa kati Philipe Mexes ambaye amekua mkaidi kwa timu hiyo katika mpango wa kubadilishana wachezaji kwa kumjikua Nicklaus Bendtner ambaye ametamka wazi kwamba hataki tena kuichezea Arsenal.
Ntajitahidi kuwajuza pindi nipatapo habari. 

Katika hali ya kushangaza Tottenham wameulizia uwezekano wa kumsajilia Marouane Chamakh kwa mkopo toka Arsenal.Timu hzo ni mahasimu wakubwa huko North London.

TAIFA STARS YAAMBULIA SARE UGENINI

Stars, Zebras Zatoka Sare
   
Friday, 17 August 2012 07:58
Stars, Zebras Zatoka Sare
Taifa Stars imetoka sare ya mabao 3-3 na wenyeji Botswana (Zebras) katika moja kati ya mechi kadhaa za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zilizochezwa leo (Agosti 15 mwaka huu) usiku.
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Molepolole ulioko Kilometa 40 nje ya Jiji la Gaborone, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa kwa penalti na beki Erasto Nyoni.
Mwamuzi Lekgotia Johannes Stars alitoa adhabu hiyo baada ya beki Oscar Obuile Ncenga wa Zebras kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akimkabili kipa Mompoloki Sephekolo.
Bao hilo halikudumu muda mrefu, kwani Zebras walisawazisha dakika ya 26 baada ya shuti kali lililopigwa na
Lemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja. Dakika tano baadaye kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars bao la pili kwa shuti la mbali.
Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37. Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto uliopigwa na Tebogo Sembowa ambaye kabla alimtoka beki Aggrey Morris.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kocha Kim Poulsen wa Stars kuwatoa Frank Domayo na Salum Abubakar na nafasi zao kuchukuliwa na Shabani Nditi na Athuman Idd. Safari hii Zebras ndiyo walioanza kufunga dakika ya 69 ambapo kiungo Michael Mogaladi aliifungia bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi fupi iliyotokana na mpira wa kurusha.
Dakika 13 za mwisho Stars walicheza pungufu baada ya beki Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu
kutokana na kumchezea rafu mshambuliaji Lovemore Murirwa.
Mrisho Ngasa ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo aliisawazishia Stars dakika ya 84 baada ya kugongeana one-two na mshambuliaji Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Moshi.
"Licha ya timu kucheza vizuri, tatizo kubwa lilikuwa kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki waliruhusu mipira mingi ya krosi na kuwaacha washambuliaji wa Botswana wakifunga bila bughudha. Mabeki hawatakiwi kuruhusu mipira ya krosi, wakiruhusu ni lazima wahakikishe wanawadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
"Kwa upande wa washambuliaji, Said Bahanuzi alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars tangu nilipomjumuisha kwenye timu kwa mara ya kwanza. Kuna makosa madogo madogo ambayo niliyatarajia, hivyo nitamrekebisha polepole," alisema Kocha Poulsen mara baada ya mechi hiyo.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo/Shabani Nditi, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar/Athuman Idd, Said Bahanuzi/Simon Msuva, Haruna Moshi/Ramadhan Singano na Mwinyi Kazimoto.
Zebras; Mompoloki Sephekolo, Tshepo Motlhabankwe/Tshepo Maikano, Edwin Olerile, Oscar Obuile Ncenganye, Mompati Thuma, Patrick Motsepe/Jackie Mothatego, Lemponye Tshireletso, Michael Mogaladi, Tebogo Sembowa, Ntesang Simanyana na Galabgwe Moyana/Lovemore Murirwa.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inarejea nyumbani kesho (Agosti 16 mwaka huu) ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Gaborone, Botswana
+26776112556
  http://www.tff.or.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=856:stars-zebras-zatoka-sare&catid=3:news&Itemid=2

MATOKEO WIKI YA KWANZA EPL

Jumapili 19/08/2012


Man City 3 - 2  Southampton

Wigan        0 - 2 Chelsea

MATOKEO YA MECHI WIKI YA KWANZA EPL

Jumamosi 18/08/2012


Newcastle   2  -  1  Tottenham   

Arsenal 0  -  0  Sunderland

Fulham 5  -  0  Norwich

QPR 0  -  5  Swansea

Reading 1  -  1 Stoke

West Brom 3  -  0 Liverpool

West Ham 1  -  0 Aston Villa
             
Santiago Carzola.Mchezaji mpya wa Arsenal ametokea kuwa usajili mzuri akionyesha mchezo mzuri katika mechi yake ya kwanza kwa timu hiyo dhidi ya Sunderland.Sunderland ambao walichukua pointi 4 msimu uliopita toka kwa walioishia kuwa mabingwa wa ligi ya Uingereza msumu uliopita Manchester City walijipanga vilivyo katika ulinzi dhidi ya madhara ya washambuliaji wa Arsenal.